0
A damaged storefront is seen after an earthquake in Halabja, IraqTetemeko la ukubwa wa 7.3 katika vipimo vya richa limekumba eneo la kaskazini mwa Iran na Iraq na kuua watu kadha.
Takriban watu 129 waliuawa katika mkoa ulio magharibi mwa Iran wa Kermanshah, kwa mujibu wa maafisa.
Tetemeko hilo lilizua hofu hadi kusababisha watu kukimbia kutoka manyumbani mwao kwenda barabarani.
Misikiti kwenye mji mkuu wa Iraq Baghdad, imekuwa ikifanya maombi kwa kutumia vipasa sauti.
Uharibifu umeripotiwa kuetka katika vijiji vinane kwa mujibu wa shirika la msalaba mwekundu nchini Iran Morteza Salim.
Baadhi ya vijiji vimekumbwa na matatizo ya nguvu za umeme na mawasiliano yamevurugwa
Makundi ya uokoaji yanatatizwa na maporomoa ya ardhi.
Tetemo hilo lilitokea kilimita 30 kusini magharibi mwa mji wa Halabja karibu na mpaka wa Iran.
Lilitokea umbali wa kilomita 33.9 na lilisikika nchini Uturuki, Israel na Kuwait.



Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top