0
Image result for redio habari njema mbuluMbali na kuhabarisha jamii na kuielimisha kupitia vipindi vyake mbalimbali vikiwemo vya dini,kituo cha redio Habari Njema  87.5 Mbulu  Manyara imeamua kuanzisha timu ya mpira wa miguu.
Kikosi hicho cha Redio habari njema Fc kinasimamiwa na kuongozwa na mwalimu aliesomea namna ya kuiweka timu katika ubora pamoja na nidhamu Filbert Mwakilambo kutoka Nchini Kenya.
Katika kukiimarisha kikosi hicho mwalimu Filbert ameamua kucheza michezo mbalimbali ya kirafiki yenye lengo la kuikusanya jamii pamoja.
Jumatano Novemba 8,2017 Habari njema Fc iliifanya kitu kibaya Boda boda Fc ya Mbulu kwa kichapo cha bao 4-2 huku wakiwatambia kuwa hayo ni kwa sababu wanawabebaga kwenye piki piki zao lakini kama sivyo wangewafunga hata bao 8.
Mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa kumbu kumbu ya Mwalimu Nyerere mtaa wa Sanu mjini Mbulu, ulihudhuriwa na mamia ya wakazi wa mji wa mbulu na viunga vyake.
Mabao yote matatu ameyafunga mchezaji machachari Ashrafu katika dakika ya 12,45 na 49 huku la nne na la ushindi likifungwa na Kasongo katika dakika ya 65.

Hata hivyo kikosi cha timu ya Habari njema Fm inayosimamiwa na Mkurugenzi Sr.Lucy Sungu kinaendelea na mazoezi kwa ajili ya michezo mingine ya kirafiki.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top