Roma inawasilisana na Manchester United kumhusu beki wa
Uholanzi Daley Blind mwenye umri wa miaka 27. (Mirror)
Viongozi wa ligi ya Serie A Napoli wameanzisha mazungumzo na
Everton kwa azma ya kusaini mkataba na mchezaji wa kati Mholanzi Davy Klaassen,
mwenye umri wa miaka 24, kwa mkopo hadi kufikia mwishoni mwa msimu. (Liverpool
Echo)
Meneja wa Newcastle Rafa Benitez amefanya mazungumzo ya
dharura na mmiliki Mike Ashley na bado ana ''matumaini'' ya kusaini mkataba
kabla ya kumalizika kwa kipindi cha kuhama wachezaji baadaye leo. (Mirror)
Lakini Benitez anasisitizia msimamo wake ambao hautarajiwi
kubadilika hata kama itashindikana kuhama kwa washambuliaji anaowalenga kama
Islam Slimani na mlinzi wa Manchester City Eliaquim Mangala (Northern Echo)
Arsenal itamruhusu mlinzi Mathieu Debuchy, mwenye umri wa
miaka 32, kujiunga na Saint-Etienne kwa uhamisho wa bila malipo. (L'Equipe - in
French)
West Ham imezungumza na Lille kuhusiana na mpango wa kusaini
mkataba na nahodha wao Ibrahim Amadou.
Crystal Palace wamekwishatoa mapendekezo mawili kwa ajili ya
mlinzi huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 24. (Sky Sports)
Wolfsburg wanajaribu kumshawishi mchezaji kiungo wa kati wa
kimataifa wa Serbia anayechezea Liverpool Lazar Markovic, mwenye umri wa miaka
23, kujiunga nao kuliko kwenda klabu ya Swansea. (Mail)
Kiungo wa kati wa Liverpool Ovie Ejaria, mwenye umri wa
miaka 20, yuko tayari kujiunga na Sunderland kwa mkopo kwa kipindi kilichosalia
cha msimu pamoja na mkabaji Mwingereza Lloyd Jones, mwenye umri wa miaka 22,
anayetaka kuhama na kuwa mchezaji wa kudumu wa Luton Town . (Liverpool Echo)
Leeds United wanakamilisha taratibu za kusaini mkataba na
mshambuliaji Tyler Roberts kutoka West Brom katika mkataba wenye thamani ya
hadi £4m. Kijana huyo mwenye umri wa miaka 19 kutoka Wales ana miezi sita
iliyosalia kwenye mkataba wake wa sasa. (Mail)
Bordeaux wako katika mazungumzo na raia wa Norway
anayechezea Rosenborg kwa ajili ya kutia saini mkataba na mshambuliaji wa
zamani wa Arsenal Nicklas Bendtner. Bendtner mwenye umri wa miaka 30 anaweza
kusaini mkataba wa awali na klabu hiyo ya Ufaransa. (TalkSport)
Baada ya kumnunua beki wa Ufaransa Aymeric Laporte kutoka
Athletic Bilbao, pesa walizotumia Manchester City kuwanunua wachezaji zimezidi
bajeti ya ulinzi ya mataifa 52. (i News)
Mipango imetangazwa ya kutengeneza filamu ya maisha ya
mshambuliaji wa zamani wa Everton Dixie Dean, ambapo Toby Kebbell anatarajiwa
kuongoza shughuli hiyo. (Liverpool Echo)
Uingereza inaweza kuwa na timu ya soka ya wanawake katika
michuano ya Olimpiki ya 2020 baada ya timu nne za nyumbani kufikia mkataba.
(Mail)
Kutoka Jumanne
Tottenham watamruhusu mshambuliaji Fernando Llorente ajiunge
na Chelsea iwapo tu watapata faida kubwa juu ya £14m walizolipa kumnunua
mchezaji huyo wa Uhispania Septemba. (Evening Standard)
Chelsea watakataa ofa zozote kutoka kwa Manchester City
kutaka kumnunua mchezaji wa Ubelgiji Eden Hazard, 27, hata kama Pep Guardiola
na klabu yake wako tayari kuvunja rekodi ya dunia ya ununuzi wa wachezaji ya
£200m. (Telegraph)
West Brom wanaongoza katika juhudi za kumtaka mshambuliaji
wa Borussia Dortmund na Ujerumani Andre Schurrle, 27, ambaye pia anatafutwa na
West Ham. (Teamtalk)
Juventus wana matumaini makubwa ya kumnunua mchezaji wa safu
ya kati kutoka Ujerumani anayechezea Liverpool Emre Can, 24, ambaye mkataba
wake utamalizika mwisho wa msimu huu. (Mail)
Post a Comment
karibu kwa maoni