Ameyasema
hayo Afisa Msajjili Wilaya (RRO) ya Ikungi mkoani Singida Bi Agnes Mtei alipokuwa anatembelea vituo vya
Usajili kuangalia maendeleo ya zoezi
linalofanyika wilayani hapo chini ya Uratibu wa ofisi ya Usajili ya
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa anayoisimamia kwa kushirikiana na Ofisi ya
Mkuu wa Wilaya - Ikungi.
Bi.
Mtei amesema kwa sasa wameshakamilisha tarafa 2 kati ya 4 zilizoko kwenye
wilaya hiyo ambazo ni: Ikungi yenye kata
za (Ikungi, Nkiwa, Isuna, Unyahati, Mangonye na Dugunyi) na Sepuka yenye kata
za Sepuka, Mwaru, Mtunduru, Igombwe, Mgungira,
Iyombo na Irisia ambapo wananchi
wameweza kufikiwa na zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa katika kata
wanazoishi.
Aidha
Bi. Mtei ameeleza kwa sasa zoezi linaendelea katika tarafa ya Ihanja katika
kata za Puma, Kituntu, Ihanja, Isokena Iglanson, Muhintiri, Makilawa,
Minyuhe na inatarajiwa kumalizika
mwishoni mwa wiki hii ndipo wataendelea katika tarafa ya mwisho iliyosalia ya
Mongaa na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi na kwa wakati kutumia fursa
hiyo kwani huduma zimesogezwa karibu katika kata na mitaa wanakoishi ili iwe
rahisi kwao kushiriki.
Mamlaka
ya vitambulisho vya Taifa inaendesha zoezi la Usajili wa mkupuo katika mikoa
takribani 16 ambayo ni pamoja na Singida, Manyara, Kilimanjaro, Arusha , Mbeya,
Njombe, Songwe, Ruvuma, Iringa, Shinyanga, Simiyu, Geita, Mwanza, Lindi, Mtwara
na Morogoro huku ikijiandaa kuingia katika mikoa ya Tabora, Dododma, Kigoma na
Kagera ambapo kwa mikoa ya Dar es Salaam,
Pwani, Tanga na Zanzibar zoezi la Usajili wa mkupuo limekamilika hivyo
wananchi wanaendelea kupata huduma mbalimbali katika ofisi ya Usajili
Vitambulisho vya Taifa katika mikoa hiyo.
Afisa Mtendaji Kata
ya Ihanja Ndg. Juma kifuda akimjazia fomu mwananchi Hassan Alli Mohamed
aliyefika kituo cha Usajili Vitambulisho vya Taifa akitokea kijiji cha Ihanja.
|
Wananchi
wa Kijiji cha Chungu wakiendelea Kusajiliwa katika kituo cha Usajili Chungu
kilichoko wilaya ya Ikungi mkoani Singida.
|
Post a Comment
karibu kwa maoni