0


SIMBA SC imesonga mbele Raundi ya Kwanza ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika kwa ushindi wa jumla wa 5-0 dhidi ya Gendarmerie Tnare ya Djibouti baada ya ushindi wa 1-0 jioni ya leo mjini Djibouti City.
Katika mchezo wa leo uliofanyika Uwanja wa El Hadj Hassan Gouled, bao pekee la ushindi la Simba limefungwa na mshambuliaji Mganda, Emmanuel Okwi dakika ya 55.
Kwa kuunganisha na ushindi wa 4-0 kwenye mechi ya kwanza jumapili ya wiki iliyopita, Simba SC inayofundishwa na kocha Mfaransa Pierre Lechantre anayesaidiwa na Mrundi, Masoud Juma, Mtunisia Mohamed Aymen Hbibi ambaye ni mchua misuli na Muharami Mohamed, kocha wa makipa inasonga mbele kwa ushindi wa 5-0 na sasa inasonga mbele kwa ushindi wa 5-0 na itakutana na El Masry ya Misri iliyoitoa Green Buffaloes ya Zambia. 
Ikumbukwe, mchezo wa kwanza El Masry iliishindilia 4-0 Green Buffaloes mjini Cairo na kesho zitarudiana nchini Zambia.
Katika mchezo wa kwanza mjini Dar es Salaam, Okwi alifunga pia bao moja, la nne baada ya kiungo Said Ndemla kufunga la kwanza na mengine mawili kufungwa na Nahodha John Raphael Bocco, aliyekosekana kwenye mechi ya leo kutokana na kuwa majeruhi.
Kikosi cha Simba SC kilichoanza leo kilikuwa; Aishi Manula, Nicholas Gyan, Asante Kwasi, Juuko Murshid, Yussuph Mlipili, Erasto Nyoni, Shiza Kichuya, James Kotei, Jonas Mkude, Emmanuel Okwi na Muzamil Yassin.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top