Katibu
wa Bunge, Steven Kagaigai amesema chombo hicho cha dola kinafuatilia
kwa ukaribu ajali ya wabunge sita iliyotokea jana usiku, Machi 29, 2018
mkoani Morogoro.
Kagaigai
amesema baada ya kupokea taarifa hizo wamefanya mawasiliano na uongozi
wa Hospitali ya Morogoro na walishauriwa kuwahamishia Hospitali ya Taifa
Muhimbili (MNH) kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
“Ndiyo
taarifa hizo ninazo, wamepata ajali huko Morogoro, tayari tumeshafanya
taratibu za kuwapeleka Muhimbili kwa huduma zaidi na ofisi yetu
inawajibika kwa kila hatua,” amesema Kagaigai.
Wabunge
hao ambao wote ni kutoka Zanzibar ni Haji Ameir Haji (Makunduchi),
Khamis Ali Vuai (Mkwajuni), Bhagwanji Maganlal Meisuria (Chwaka), Makame
Mashaka Foum (Kijini), Juma Othman Hija (Tumbatu).
Post a Comment
karibu kwa maoni