0
Image result for sheikh amri abeid memorial stadium 
TIMU za wanawake na wanaume za Future stars na Monduli Coffee zimefanikiwa kuibuka na ubingwa katika bonanza la  soka lililoshirikisha makampuni na taasisi mbalimbali.
Katika mchezo wa fainali kwa wanawake timu ya Future Stars ilifanikiwa kuichapa timu ya Elewana Sopa kwa jumla ya mabao 6-0, huku kwa wanaume timu ya Monduli Coffee iliichakaza  timu ya Arusha Stars kwa mabao 3-2. Michezo yote ikichezwa katika uwanja wa TGT nje kidogo ya jiji la Arusha.
Jumla ya timu ishirini kutoka taasisi mbalimbali zilishiriki bonanza hilo lilioandaliwa na taasisi ya kukuza na kuinua vipaji kwa vijana ya Future Stars ambapo washindi walizawadiwa vikombe.
Mkurugenzi wa taasisi ya future Stars Alfred Itaeli alisema bonanza hilo ni awamu ya nne kufanyika huku hamasa ikiongezeka kwa washiriki kujitokeza.
"Sisi kama waandaaji tunajivunia kukutanisha watu  maana hii pia ni katika Sera ya serikali kufanya mazoezi pia kusisitiza michezo na hii inajenga watu kiafya na kujumuika pamoja katika kujenga mahusiano Mapya baina ya taasisi na makampuni na tunatarajia tena mwezi wa sita kukutana ," alisema Itaeli.
Kwa upande mchezaji kutoka kampuni ya Elewana Sopa,Millika Mumba alisema michuano ilikuwa na ushindani  na ikizingatiwa ni mara ya kwanza kushiriki na kuwasihi waandaaji kuendelea kuandaa tena na wanawake wajitokeze.
Naye mchezaji James Wambura kutoka Future Stars alieleza kuwa bonanza hili pia limekutanisha wachezaji wa zamani na wameonyesha jinsi walivyokuwa wakisakata soka .

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top