0
Leo March 24, 2018 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Avemaria Semakafu ametoa ufafanuzi kuhusu utata ulioibuka kuhusu kigezo cha umri wa kujiunga na masomo ya kidato cha tano na sita na kusema taarifa ambayo imesambaa imekuwa na makosa.
Semakafu amesema kuwa yametokea makosa wakati wa uandishi ila kujiunga na masomo ya kidato cha tano na sita ni miaka 25 na siyo miaka 20 kama ambavyo inasomekana katika taarifa iliyotolewa jana.
“Kumetokea makosa ya kiandishi, miaka ni 25 ya kujiunga sekondari na sio 20 kama ambavyo inasomeka kwenye ile karatasi” -Dkt. Semakafu 

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top