0
Kutoka nchini Uganda, siku ya jana March 23, 2018 wafungwa watatu wamehitimu masomo yao ya shahada ya kwanza ya masomo ya sheria katika Gereza Kuu la Luzira jambo ambalo ni jipya kwa nchi nyingi za Afrika.
Wafungwa hao Pascal Kakuru, Suzzan Kigula na Moses Ekwam walionekana wamevaa majoho ya mahafali kama walivyo wahitimu wengine.
Kuhitimu kwa wafungwa hao kumefanikishwa na mradi maalumu kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha London wa kuwapa wafungwa fursa ya kupata elimu wakiwa kwenye kifungo, ikiwa ni kutimiza haki yao ya msingi.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top