0
Chama cha soka  mkoa wa Manyara (MARFA) kimepanga kuzishusha daraja timu zake tatu ambazo zilikuwa zipo katika ngazi ya mkoa baada ya mwaka huu kushindwa kushiriki ligi hiyo bila sababu maalum.
Akiongea na championi jumatatu katibu wa mashindano wa chama cha soka mkoa wa Manyara (MARFA) Yusuph Mdoe alizitaja timu hizo kuwa ni Galapo parish fc ya Babati,Songa fc na Mererani Sports kutoka Mirerani wilayani Simanjiro.
Alisema wao kama chama cha soka mkoa walitoa barua mapema inayoelezea tarehe ya kuanza kwa ligi ya mkoa lakini mpaka inaanza timu hizo azikupeleka barua ya kuthibitisha kushiriki hivyo hatua ambayo wanatarajia kuchua ni kuzishusha kutoka ligi daraja la tatu ngazi ya mkoa hadi ligi daraja la nne ngazi ya wilaya.
"Mpaka sasa hatuna taarifa yoyote kuhusu timu hizo kwa nini azijashiriki na kanuni hiko wazi kama timu aijashiriki basi inakuwa imejishusha tena mpaka ngazi ya wilaya lakini pia kama kamati ya mashindano tutakaa kuona ni hatua gani tena tuzichukue kwa timu hizi" alisema Mdoe.
Akizungumzia  ligi ya mkoa ambayo inaendelea sasa katika uwanja wa chuo cha ufundi Nangwa wilayani Hanang alisema timu zinazoshiriki mwaka huu zimejipanga kwani kuna ushindani mkubwa tofauti na msimu uliopita.
Alisema ligi hiyo inashirikisha timu kumi katika makundi mawili ya A na B kila kundi ikiwa na timu tano ambazo zinachuna vikali kutafuta timu tatu kutoka kila kundi zitakazo tinga hatua ya sita bora.
Kundi A kuna timu za Babati Mashujaa sc,Morning Star fc,Fire stone fc,Magugu rangers fc na Gwadaat fc,
Kundi B kuna timu za Usalama Sc, Halmashauri fc, Mrara fc,Nangwa fc na Red star fc.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top