0
Image result for DC HANANG 
Mkuu wa wilaya ya Hanang Sara Msafiri katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani amekemea wanawake wilayani humo na mkoa kwa ujumla kuwa kama chambo cha kutumika katika migogoro inayoendelea wilayani humo.

Alisema  wanawake wamekuwa wakitumika katika migogoro mingi ya vijiji na jamii  katika wilaya ya hanang na mkoa wa Manyara kutokana na mila na desturi walizorithi kutoka enzi za mababu. 
 
Alibainisha hayo  katika mahojiano maalum na WALTER HABARI kuhusu kuelekea siku ya wanawake duniani (Leo) ambapo aliwataka wanawake wa wilaya hiyo kubadilika na kuachana na mkila potofu na badala yake kujihusisha na masuala ya kimaendeleo. 

Alisema  kutokana na mila na desturi za makabila kutoka wilaya ya Hanang na mkoa wa Manyara kwa ujumla kuna mila zinazofanana ambapo wanawake wamekuwa wakitumika sana kwenye maandamano na  migomo. 

“Kama Mwenyekiti wa ulinzi na usalama wa wilaya hii nimeshuhudia migogoro mingi inayotokana na chimbuko hilo la mila na desturi, mila ambazo zimepitwa na wakati kwenye vijiji au jamii wanawake wanatumika”.Alisema.
Akitolea mfano wa wanawake waliowahi kaa nje kwa mgomo kuhusu matumizi ya ziwa Bassuto ambapo wapo wananchi wanaoamini kuwa ziwa hilo kuabudu kwa masuala ya kimila na wapo wanaokuwa wanataka matumizi ya ziwa hilo kwa masuala ya kiuchumi, Uvuvi na umwagiliaji ambapo wanawake hao waligoma na kulala nje kwa muda wa miezi mitatu. 

“Nikiwa nimeteuliwa kushika nafasi hii mwaka 2016 nikakuta wanawake hao wameshakaa nje miezi mitatu katika kipindi cha baridi cha kipimajoto 684 wanawake walikuwa wakikohoa huku wanaume wakiwa majumbani kwao wanawatuma wanawake hao kugoma” Alisema. 

Aliongeza kueleza kuwa migogoro mingine  imeshawahi kutokea katika maeneo ya shughuli za uchimbaji wa madini na mgodi wa chumvi wa Gendabi wanawake zaidi ya 400 walishawahi kukaa nje zaidi ya wiki tatu kugoma na hawataki kufuata taratibu mbalimbali za kusikiliza kero zao katika vikao huku wanaume wakiwa majumbani kwao. 

Aliwaasa wanawake wote wa wilaya ya Hanang na mkoa wa Manyra kuelekea siku  ya mwanamke duniani kujielekeza nguvu zao katika shughuli za uzalishaji za kijamii ili kukuza kipato na kusomesha watoto wao badala ya kutumiwa kama chambo cha  kuhamasisha maandamano. 

Pia wanawake hao wahakikishe kuwa wanapata haki ya kumili ardhi,mali na kwamba wasitumiwe tu akawa kama mtoto wa kwanza katika familia kwani kuna kesi nyingi zinazobainisha wanawake wanaachika katika ndoa zao wakiwa na watoto wanaowatunza bila kuachiwa chochote cha kurithi. 

“Pale ndoa zinapovunjika mwanamke upate haki zako katika vyombo vya sheria, katika dawati la jinsia na kupata ushauri katika ofisi za  mkuu wa wilaya na taasisi za kisheria zinazosaidia wanawake.” 

Aidha aliwaasa kubadilika na kujielekeza katika uzalishaji na kuacha kutumiwa kama chombo cha kufanya migomo isiyo na tija.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top