0


Image result for ESTER MAHAWEWabunge wa viti maalum Ccm mkoa wa Manyara Ester Mahawe na Martha Umbura wametimiza ahadi yao ya kuwapatia vifaa vya shule watoto yatima 43 wanaosoma katika shule ya msingi Bonga iliyopo Babati ahadi walioitoa Februari 2 mwaka huu baada ya kufanya ziara shuleni hapo katika kuazimisha miaka 41 ya kuzaliwa kwa chama hicho.
Katibu wa umoja wa Wanawake Tanzania UWT mkoa wa Manyara Haines Munisi akiwa na viongozi wengine wa chama hicho Mapema mwezi Februari waliwatembelea wanafunzi hao na kuwapatia misaada mbalimbali na kuwafikishia jambo hilo wabunge hao.
Mwandishi wa habari hizi alishuhudia majengo chakavu yaliyojengwa zamani kwa udongo yakiendelea kutumika hadi leo na wanafunzi 1,037 huku mkuu wa shule ya msingi Bonga January Barnabas akiwaomba wabunge hao Ester Mahawe na Martha Umbura kutatua changamoto hizo.
Wabunge  hao wa Ccm mkoa  wa Manyara Ester Mahawe na Martha Umbura wamesema kuwa wanaendelea na utekelezaji wa ilani ya chama chao katika kuwahudumia wananchi.
Vifaa vya shule vilivyokabidhiwa ni sare za shule,viatu,madaftari pamoja na kalamu.
Pamoja na hayo Mbunge Martha Umbura alisimamia harambee ya kuwachangia wanafunzi kuweza kupata chakula cha mchana huku waandishi wa habari waliombatana katika msafara huo wakigusawa na kutoa michango yao ambapo zilipatikana gunia 12 za mahindi,debe 12.5 za maharage,mafuta ya kupikia lita 60,chumvi katoni 2 na shilingi 20,000.
Kwa pamoja wamekubaliana kuwa ahadi hiyo kutimizwa ifikapo april 2 mwaka huuu siku ya jumanne.
Katika hatua nyingine Mbunge Ester Mahawe amehamia jimbo la Babati mjini akieleza kuwa ni kuwatumikia wakazi wa jimbo hili linalokaliwa na Mbunge upinzani [CHADEMA] Paulina Gekul.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top