0

Related imageMchezo kati ya Mtibwa Sugar na Simba Juzi ulioipa  ushindi Simba Sc katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kuwachapa wenyeji, Mtibwa Sugar 1-0 Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro umemsababishia majeraha kijana mmoja mjini Babati.
Kamanda wa polisi mkoa wa Manyara akizungumzia tukio hilo ameeleza kuwa limetokea tarehe 9.4.2018 saa tatu usiku ambapo Mtuhumiwa huyo aliefahamika kwa jina la Stefano Festo [35] mkazi wa Hangoni C alimjeruhi mhudumu wa Bar ya Toroka Uje mtaa wa Osterbay  Daniel Elia baada ya kuzuka mabishano ya ushabiki wa mpira mechi  kati ya Mtibwa Suga na Simba Sc .
Kijana huyo ambaye ni shabiki wa Simba alikuwa akishangilia ushindi walioupata jambo ambalo lilimkera Daniel  anaeaminika kuwa ni shabiki wa Yanga na kuamua kumponda kwenye paji la uso na mtwangio wa Kinu na kumsabishia Maumivu makali.
Kamanda Senga amesema mtuhumiwa bado anashikiliwa katika kituo cha polisi mjini Babati kwa hatua nyingine za kisheria.
Daniel aliejeruhiwa anaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu katika hospitali ya mji wa Babati Mrara.
Ushindi huo wa juzi  unaifanya Simba SC ifikishe pointi 52 katika mechi ya 22 ikiendeleza kuongoza Ligi Kuu kwa pointi sita zaidi ya mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 46 za mechi 21, wakati Mtibwa Sugar inabaki katika nafasi ya sita na pointi zake 30 za mechi 22 pia.
Bao hilo lilifungwa na mshambuliaji Mganda, Emmanuel Arnold Okwi dakika ya 23 kwa shuti akiwa ndani ya boksi baada ya pasi ya kichwa ya Nahodha John Raphael Bocco aliyeunganisha krosi ya winga Shiza Ramadhani Kichuya.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top