Jeshi
la Polisi Mkoa wa Mtwara, linawashikilia wanafunzi tisa wa Chuo Kikuu
cha Stella Maris na Daktari wa Hospitali ya Mission Nanyamba kwa tuhuma
za kumkashifu Rais John Magufuli na kuhamasisha maandamano ya Aprili 26.
Akizungumza
na waandishi wa habari Jumamosi, Kamanda wa Polisi mkoani humo, Lucas
Mkondya, alisema watuhumiwa hao kwa nyakati tofauti wamekuwa wakitumia
mtandao wa kijamii wa WhatsApp na Telegram kumkashifu Rais na
kuhamasisha maandamano hayo.
Kamanda
Mkondya bila kutaja majina ya watuhumiwa hao kwa madai ya sababu za
kiupelelezi, alisema daktari huyo ni kutoka Halmashauri ya mji wa
Nanyamba.
“Ninatoa
onyo watu wajiepusha kutumia mitandao ya kijamii vibaya na kusababisha
uvunjifu wa sheria za nchi. Watuhumiwa wote tunawashikilia kwa upelelezi
zaidi,” alisema.
Katika
tukio lingine, Kamanda Mkondya alisema wanawashikilia wahamiaji haramu
23 waliokutwa katika nyumba ya kulala wageni eneo la Chikongola, Wilaya
ya Mtwara.
“Wahamiaji
hawa wanatoka nchi tatu tofauti, 13 kutoka nchi ya Demokrasia ya Congo,
saba kutoka Rwanda na wawili kutoka Burundi, katika mahojiano wamesema
walikuwa wakielekea Ufaransa kwa kupitia visiwa vya Comoro,” alisema.
Pia
alisema wanawashikilia watu 13 ambao wanajihusisha na mtandao wa wizi
wa pikipiki katika kijiji cha Chikongo, wilayani Tandahimba.
Kamanda Mkondya alidai kuwa mtandao wa wezi hao unaongozwa na Mohamed Juma (simba).
Post a Comment
karibu kwa maoni