0
Responsive imageWizara ya Nishati imewataka wakandarasi wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini (REA) katika awamu ya tatu kukamilisha miradi hiyo ifikapo june 2019 na kwamba serikali  haitaongeza muda kwa wataoshindwa kukamilisha kazi hiyo kwa muda uliopangwa.
Hayo yamesemwa na Waziri wa nishati Dokta Medard Kalemani wakati alipotembelea na kukagua utekelezaji wa miradi ya REA katika wilayani za Same na Siha mkoani Kilimanjaro.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Same, Rosemary Senyamule amesema mradi huo utasaidia kukabiliana na changamoto ya umeme iliyokuwa ikiwakabili wananchi wilayani humo.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top