0
Mdudu tishio kwa wakulima.

Wakulima wameeleza hatari ya kukubwa na Baa la njaa kutokana na kuibuka kwa wadudu wanaoshambulia zao la mahindi na maharage.

Wakizungumza na WALTER HABARI wakulima hao kwa nyakati tofauti wameeleza kuwa wadudu ambao hawafahamiki kwa majina, wamejaribu kutumia madawa mbalimbali bila mafanikio hali inayowapa wasiwasi mkubwa wa kukosa chakula.

Wamesema wadudu hao wanaofanana kama wale  Viwa vijeshi wanatafuna kati kati ya kiini cha mmea haswa mahindi na maharage na kuyazuia kukua.

Walter Habari imetembelea baadhi ya mashamba mkoani Manyara na kushuhudia mahindi yakiwa yameharibiwa na wadudu hao.

Baadhi ya Maeneo niliyoyatembelea ni Komoto,Daghailoy,Gadwet na Kona ya Nakwa Bagara.
 Pia wakulima hao wameiomba wizara kuweza kudhibiti madawa feki ambayo hayana msaada kwao,yamekuwa yakiwapatia hasara mara nyingi.
Wizara ya kilimo  kupitia kwa afisa kilimo mkuu Serigijuan  Mtaiwa akimzungumzia mdudu huyo amewataka wakuli ma na wataalamu wa kilimo kukagua mazao mara kwa mara.

Afisa kilimo mkuu amesema kuwa Mdudu huyo ni mgeni hapa nchini  aliingia nyanda za juu kusini mkoa wa Rukwa katika wilaya ya Nkasi march 2017 na mpaka sasa tayari ameshaenea maeneo mbalimbali ya Tanzania Bara.

Amesema mdudu huyo anatokana na Nondo[Kipepeo] wanaoonekana majira ya usiku na hutaga mayai chini ya jani ya mmea na mayai huanguliwa baada ya siku tatu na kutoa viwavi ambavyo vinafanya uharibifu wa mazao na baadae kuwa Buu na kujichimbia chini na kugeuka kuwa kipepeo.

Wizara imeanza kutembelea mikoa mbalimbali na kutoa elimu kwa wataalamu wa kiulimo ili wafikishe elimu hiyo kwa wakulima namna ya kumdhibiti mdudu huyo.
Rangi yake ni Kijivu.
 
Anakaa kati kati ya kiini cha Mhindi.

Akishatafuna kiini cha Muhindi anasaga na kuacha pumba pumba na pia anataga Mayai.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top