BABATI
Na
John Walter
Vijiji
vitano vya wilaya ya Babati mkoani Manyara vinatarajia kunufaika namradi mkubwa
wa maji utakaogharimu shilingi bilioni moja.
Akizungumza
na kituo hiki mhandisi wa maji halmashauri ya wilaya ya Babati Onesmo Joachim
amesema kuwa kukamilika kwa mradi huo unategemea fedha kutoka serikali kuu.
Amesema kuwa
utekelezaji wa mradi huu ulishaanza mapema mwaka huu ukasimama kwa muda
kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha hali iliyopelekea ziwa kujaa na
kusababisha kushindwa kupitisha mabomba ambayo yanapitia pembezoni mwa ziwa
hilo kwa kutumia teknolojia ya kisasa inayotumika katika nchi zilizoendelea.
Ameeleza
kuwa maji wanayachukua kutoka katika
kijiji cha Moya maghara kupeleka maji katika vijiji vitano kupitia kando ya
ziwa manyara ambapo utavisaidia vijiji
vitano ikiwemo minjingu,Kakoi,Olasiti,Vilima vitatu na Ngorei vinavyokabliwa na
uhaba mkubwa wa maji.
Mradi huo
unatarajia kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.
Amewataka
wanakijiji hao waendelee kutoa mchango wao ili kufanikisha zoezi hilo ambalo
limelenga kuwatoa katika adha ya maji wanayokabiliana nayo.
Post a Comment
karibu kwa maoni