Leo nimezunguka katika majimbo ya Mbeya Vijijini ,Vwawa na Tunduma nikiwaeleza kuhusu Operation UKUTA,
UKUTA
si fujo , UKUTA si machafuko na hatuna haja ya kufanya fujo , tunapiga
kelele dhidi ya uvunjwaji wa haki ya kidemokrasia na katiba ya nchi
unaofanywa na utawala huu wa awamu ya tano .
CHADEMA
ni nani wakapambane na polisi ,polisi ambao ni watoto wetu ,ndugu zetu
na hata wake na waume zetu ila tuwahakikishie hatutorudi nyuma pale
katiba na haki ya kidemokrasia ikichezewa au kuwa chini ya mtu fulani .
Najua
polisi watapiga watu ,wataumiza watu na hata kuua ila niwahakikishie
wao na walio na mamlaka wataishia katika mahakama ya Kimataifa .
Siasa
ni mazungumzo ,lazima tuzungumze milango yetu iko wazi kufanya
mazungumzo ila kwa kuwa hawahitaji na sisi hatutorudi nyuma September
Mosi ,tumejiandaa vya kutosha na sasa tuko ngazi ya kaya na wajumbe wetu
wanakamilisha kazi katika kaya ili tarehe mosi sauti ya kutosha ipazwe
kwa maandamano na mikutano kama tulivyokubaliana katika kata zetu na
majimbo nchi nzima .
Haiwezekani hata kidogo mtu mmoja azuie kila kitu ,nchi hii ni mali yetu sote na inaongozwa na Katiba na sheria.
Kamati
kuu ilipoamua katika suala la UKUTA haikukurupuka , kamati kuu yetu
inaundwa na mchanganyiko wa wasomi wa kada mbalimbali ,wazee wenye
busara na vijana machachari kamwe hawawezi kukukurupuka na UKUTA ni haki
ya watanzania wote.
Pili
naomba niwape siri ya ushindi 2020 ndugu zangu na wanachama wenzangu ,
tutashinda uchaguzi Mkuu 2020 kama tutafanya yafuatayo na kuyasimamia
Kwanza; Umoja ndani ya Chama na wanachama ,tuheshimiane ,tusameheane na tuimarishe chama chetu
"chama ndani ya Chama , chama nje ya chama na chama ndani ya Umma "- LOWASSA
Post a Comment
karibu kwa maoni