Chama cha Demokrasia na Maendeleo [Chadema]
kimetoa salaam za pole kwa wananchi wote walioathirika na tetemeko la
ardhi katika maeneo ya mikoa ya Kagera, Mwanza, Tabora na kwingine,
tukio ambalo limesababisha vifo vya watu 16, majeruhi na uharibifu
mkubwa wa mali.
Kupitia
taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Idara ya Habari ya Chama hicho, Tumaini
Makene, chama hicho kimetoa wito kwa Watanzania wote katika maeneo
yaliyopatwa na tetemeko hilo na wengine kutoka nje ya sehemu hizo,
kuguswa na tukio hilo na kuwiwa kuwasaidia waathirika wa tukio hilo
katika wakati huu mgumu wa kukabiliana na athari zilizotokana na janga
hilo.
Imesema
viongozi wa chama katika ngazi mbalimbali, wabunge, madiwani na
wanachama wote wa Chadema wataungana na kusaidiana kwa kila hali na wote
walioathirika na tukio hilo.
Post a Comment
karibu kwa maoni