Idadi ya watu waliouawa kwenye,
mlipuko mkubwa wa bomu katika eneo lenye shughuli nyingi kwenye mji mkuu
wa Somalia Mogadishu siku ya Jumamosi, imefikia watu 300 hadi sasa, kwa
mujibu wa ripoti ya shirika la habari la Reuters
Takriban watu
wengine 300 walijeruhiwa kwa mujibu wa AFP, wakati lori lililokuwa
limejazwa vilipuzi lilipolipuka karibu na lango la hoteli.Reuters walimnukuu Ahmed Ali, mwuguzi anayefanya kazi kwenye hospitali moja akisema kuwa miili 160 haikuweza kutambuliwa na hivyo ilizikwa na serikali jana.
Anasema kuwa miili mingine ilizikwa na jamaa zao.
Hilo ndilo shambulizi baya zaidi kutokea nchini Somalia tangu kundi la al-Shabab lianzishe harakati zake mwaka 2007.
Watu waliandamana kupinga mauaji hayo. |
"Tumethibitisha kuwa watu 300 waliuawa kwenye mipuko huo. Idasi ya waliokufa huenda bado ikaongezeka na kuna watu kadha ambao bado hawajulikani waliko," Abdikadir Abdirahman, mkurugenzi wa idara ya magari ya kusafirisha wagonjwa aliliambia shiria la Reuters.
Post a Comment
karibu kwa maoni