0
Wakuu wa wilaya na wenyeviti wa Halmashauri za wilaya za mkoa wa MANYARA wamesema kuwa migogoro mingi ya kiutendaji katika wilaya zao inatokana na viongozi hao kuingiliana kiutendaji kwa kutojua mipaka yao.
Mkuu wa mkoa wa MANYARA, DKT. JOEL BENDERA
Wakuu wa wilaya na wenyeviti wa Halmashauri za wilaya za mkoa wa MANYARA wamesema kuwa migogoro mingi ya kiutendaji katika wilaya zao inatokana na viongozi hao kuingiliana kiutendaji kwa kutojua mipaka yao.

Wakizungumza  wakati wa semina elekezi ya viongozi na Watendaji wa Halmashauri za mkoa wa MANYARA, baadhi ya Wakuu wa wilaya na Wenyeviti wa Halmashauri hao wamesema kuwa kutojua mipaka ya kiutendaji ya Serikali kuu na Serikali za mitaa kumesababisha migogoro katika wilaya zao.

Akizungumza wakati wa semina hiyo, Mkuu wa mkoa wa MANYARA DKT.JOEL BENDERA amesema kuwa mkuu wa shughuli zote za Serikali katika wilaya ni mkuu wa wilaya na amewataka Madiwani na Watendaji katika Halmashauri mkoani humo kuacha mivutano.

Post a Comment

karibu kwa maoni

Top