Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma imevuna jumla ya wanachama wapya 102 kutoka chama cha Act Wazalendo na Chama cha Wananchi Cuf.
Wanachama
hao ambao wamepokelewa na mjumbe wa halmashauri kuu ya Chama cha
Mapinduzi Mkoa wa Kigoma Prof Joyce Ndalichako ambaye aliwakabidhi
wanachama hao wapya kadi 102 , akiwemo Mwenyekiti wa Chama cha ACT
wazalendo Wilaya ya Kakonko pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha wananchi
CUF Wilayani humo .
Zoezi
hilo alilifanya jana katika Sherehe za maadhimisho ya Miaka 40 ya Chama
Cha Mapinduzi Wilaya ya Kakonko, ambapo Wanachama kutoka katika Vyama
vya ACT wazalendo, NSSR Mageuzi, CHADEMA na Chama cha Wananchi CUF ambao
waliamua kuvihamba Vyama hivyo kutokana na Waanzilishi wa Vyama hivyo
kukosa uzalendo kwa Nchi yao kwa kuwashawishi viongozi walio chaguliwa
na vyama hivyo kuipinga Serikali katika masuala ya Maendeleo.
Sambamba
na zoezi hilo Ndalichako aliwaomba Wanachama Wa CCM Wilayani humo
katika uchaguzi wa viongozi wa Chama 2017 kuhakikisha Wanachagua
viongozi wazalendo Wanaoweza kukijenga chama katika Misingi ya Uzalendo,
amani na mshikamano kama Waanzilishi wa Chama hicho walivyo kijenga
Chama hicho ambacho kinazidi kuwa ni Chama kinacho wajali wanyonge.
Alisema
Kauli mbiu ya maadhimisho ya Miaka 40 ya Chama Cha mapinduzi ni CCM
mpya na Tanzania mpya .kauli hiyo haiwezi kukamilika endapo chama hicho
kitapata viongozi wasaliti wasio na mapenzi na Chama ambao wengi wao
wametumika kununuliwa na vyama vya upinzani katika kipindi cha uchaguzi
wa mwaka 2015 ambapo CCM imepoteza majimbo wengi kutokana na viongozi
hao waliokisaliti Chama.
"Nianze
kwa kuwapongeza Wanachama walio amua kurudi katika Chama cha Mapinduzi
wamefanya jambo zuri sana, CCM ni chama ambacho kikitoa ahadi zake
lazima zikamilike na ni chama chenye misingi ya uwajibikaji, uzalendo
amani na ushirikiano ndio maana Wananchi wengi wanaendelea kukiamini
chama chetu kutokana nuwaombe Wanachama Wenzangu tusikubali kurubuniwa
na baadhi ya watu wasio kipenda chama kikiuka Misingi ya Waanzilishi Wa
chama chetu walioiweka ambayo inatusaidia Chqma hiki kuwa na Amani na
mshikamano tofauti na Vyama vingine", alisema Ndalichako.
Kwa
upande wake Katibu Wa Chama cha Mapinduzi Mkoa Wa Kigoma,Naomi
Kapambala aliwashukuru Wanachama hao kwa kukiamini Chama hicho na kuamia
kujiunga! Aliwaahidi Wanachama hao kuwa Chama hicho kitaendelea kutenda
haki na kuwatumikia Wananchi katika misingi ya uwajibikaji na
kujitegemea ilikuhakikisha Chama hicho kirudisha misingi yake ya zamani.
Hata
hivyo Kapambala aliwaomba wanachama wote kuendelea kudumisha Umoja na
mshikamano katika kuhakikisha Shughuli za chama hicho zinasonga mbele na
Kwa kipindi cha uchaguzi wa mwaka 2017 wahakikishe Wanachagua viongozi
Waadilifu,wasio penda rushwa na wanaotumiwa katika kukidhohofisha chama
kutokana na maslahi ya baadhi ya Watu wasio penda Maendeleo ya Chama
hicho.
Nao
baadhi ya Wanachama walio hamia CCM, akiwemo Mwenyekiti wa ACT
wazalendo Nikolaus Weslaus alisema ameamua kukihama chama hicho kutokana
na Mapungufu yaliyomo katika Chama hicho, alisema kunamambo aliyo
yagundu katika chama hicho ni kitu kimoja kinaanzia kwa viongozi wa Juu
wavyama vya upinzani unaoleta msukumo Mkubwa kwa wanasiasa wake na
wananchi ili Nchi hii isiweze kutawaliwa ikiwemo zoezi la kuwashawishi
madiwani na Wabunge kupinga kila kitu kinachoendelea katika Serikali
hata kama ni cha maendeleo bila sababu ya Msingi.
Alisema
Ameamua kuhamia CCM kutokana na Rais aliyepo madarakani anasisitiza
suala la uwajibikaji na vita dhidi ya rushwa ambavyo vimekuwa vikwazo
vikubwa vya kuzuia maendeleo ya Nchi hii na Zoezi hilo linaendelea
Kukamilika bila shida yoyote na serikali inaendelea kuwahudumia wananchi
wote kwa usawa bila kuangalia chama.
Amana
Ramadhani ni Mwenyekiti wa Chama cha wananchi CUF Wilaya ya Kakonko
alisema ameingia kwenye chama hicho tangu mwaka 1997 kutokana na chama
hicho kuwa na sera nzuri na kwakuwa na malengo mazuri ya kuisaidia
Serikali katika kupata Suqla zima la Demokrasia pamoja na maendeleo,
lakini mpaka sasa kitu alicho kitalajia katika Chama hicho hajakiona.
Na
kilicho mfanya kuhamia CCM ni baada ya kuona Serikali ya Awamu ya Tano
inavyo tekeleza Ilani yake kama ilivyo ahidi kipindi cha Kampeni na Sasa
wanaendelea kuitekeleza kauri ya hapa Kazi tuu ambayo faida yake
wanaiona mpaka sasa , ambapo kila idara ya Serikali inafanya kazi yake
ipasavyo tofauti na Vyama vya upinzani hakuna kazi nyingine wanayo
ifanya zaidi ya malumbano.
Katika
Sherehe za kuadhimisha miaka 40 Wilaya ya Kakonko ilifanya shughuli za
Kufanya usafi Wa Zahanati ya Wilaya hiyo, kufungua ujenzi wa Ofisi ya
Chama cha Wilaya pamoja na kikao cha Wanachama kilicho husisha upokeaji
wa Kadi kutoka kwa Wananchama wapya wa CCM
Post a Comment
karibu kwa maoni