0
Wanakijiji wa kijiji cha King'ori Arumeru mkoani Arusha wanalazimika kununua maji shilingi 600-1000 kwa ujazo wa lita ishirini kwa kutokana na kukatiwa maji na kijiji jirani cha Ngwasenga huku wakiwatishia kuwadhuru endapo watajaribu kwenda katika kijiji hicho kwa dhumuni la kutaka maji.
Kwa mujibu wa taarifa za uhakika kutoka katika kijiji hicho Viongozi mbalimbali wameshafuatilia na jitihada zao zote zimekwama wakielezwa kwamba hata wamfikishie taarifa hizo rais John Magufuli hawataruhusu maji kwenda King'ori.
Kwa sasa maji wanayapata kupitia visima vya asili tena katika umbali mrefu na kutembezewa kwa Maboza kwa gharama kubwa.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top