
Akizungumza
na Waandishi wa Habari, katika Ofisi za Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu
zilizopo Fumba kisiwani Unguja, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga
Joelson Mpina amesema pamoja na meli hizo kuamriwa kulipa faini ya
Shillingi Billioni moja (Tshs. 1,000,000,000) kila moja zinatakiwa
kurejea katika bandari za Tanzania kwa ajili ya ukaguzi kwa kuwa leseni
zao bado hazijaisha muda wake hadi sasa ili kubaini thamani halisi ya
kiasi cha fedha zitakazotozwa kwa ajili ya samaki waliovuliwa bila
kukusudia(Bycatch).
Aidha
Mpina amesema meli hizi zimetakiwa kuilipa Tanzania kiwango cha pesa
kwa mujibu wa soko la kimataifa kutokana na kuondoka na Bycatch
waliyoripoti kuwa wanayo kabla ya kutoroka.
Waziri
Mpina amemuagiza Katibu Mkuu Uvuvi, Dkt. Yohana Budeba kuiamru Mamlaka
ya uvuvi wa Bahari Kuu (DSFA) iwaandikie notisi wahusika wa meli hizi
kuwajulisha kuhusiana na maamuzi haya pia kuwajulisha Kamisheni ya
Jodari kwenye Bahari ya Hindi, (IOTC) kuhusiana na hatua zilizochukuliwa
na Tanzania dhidi ya meli hizo ili isaidie kuwabaini na kuwachukulia
sheria kwa mujibu wa Sheria husika.
Aidha
imeamriwa kwamba Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu pia iandae barua/
andiko kwa Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi ili aweze kuiandikia
Barua Wizara ya Mambo ya Nje kwa lengo la kuwasiliana na Flag States
(Mataifa ambayo meli hizi zimesajiliwa) ili kuwajulisha makosa
yaliyotendwa na meli husika pamoja na hatua ambazo Tanzania imechukua.
Amesema meli zote zilizotoroka zimesajiliwa nchini China.
Wakati
huo huo Waziri Mpina amesema meli ya Tai Hong 1 imekiuka Kifungu cha
18 cha Sheria ya uvuvi wa Bahari kuu No. 1 ya Mwaka 1998 na marekebisho
yake ya mwaka 2007 pamoja na Kanuni ya 66 ya kanuni za uvuvi wa Bahari
kuu za Mwaka 2009 na marekebisho yake ya mwaka 2016 kwa kukutwa na
mapezi ya papa yasiyoendana na miili iliyokutwa kwenye meli hiyo baada
ya kukaguliwa katika bandari ya Dar es Salaam mnamo tarehe
25/01/2018-27/01/2018.
Pia
meli hii imebainika kukiuka kanuni ya 10 ikisomeka pamoja na kanuni ya
68 ya kanuni za uvuvi wa Bahari Kuu za mwaka 2009 pamoja na marekebisho
yake ya mwaka 2016 kwa kuhaulisha mabaharia kutoka kwenye meli nyingine
ambao idadi yao ilikuwa mabaharia 10.
Aidha
meli hii pamoja na kukutwa na makosa hayo iliondoka nchini bila kufuata
taratibu zinazotakiwa kwa mujibu wa vifungu tajwa hapo juu.
Kutokana
na makosa hayo imeamriwa na Mamlaka ya Bahari kuu (DEEP SEA FISHING
AUTHORITY) kulipa jumla ya faini ya Shillingi Billion moja (Tshs.
1,000,000,000) ambapo Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu itawasilisha notisi
ya adhabu hii kwa wahusika wa Meli hii ya TAI HONG 1.
Mbali
na Tai Hong 1 Mpina amezitaja Meli hizo zilizopigwa faini ya Bilioni
moja kila moja kuwa ni pamoja na TAI HONG NO2 yenye namba ya leseni
TZ/DSFA/EEZ/453, TAI HONG 8 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/454, ,TAI
XIANG 2 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/455, TAI XIANG 5 yenye
namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/456, TAI XIANG 1 yenye namba ya leseni
TZ/DSFA/EEZ/457, TAI XIANG 8 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/458 na
TAI XIANG 9 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/459.
Meli
nyingine ni TAI XIANG 10 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/460, TAI
XIANG 7 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/461, TAI XIANG 6 yenye namba
ya leseni TZ/DSFA/EEZ/462, TAI HONG 6 yenye namba ya leseni
TZ/DSFA/EEZ/463, TAI HONG 7 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/464, XIN
SHIJI 81 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/466, XIN SHIJI 82 yenye
namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/467, XIN SHIJI 83 yenye namba ya leseni
TZ/DSFA/EEZ/468, XIN SHIJI 86 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/470,
XIN SHIJI 72 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/471, XIN SHIJI 76 yenye
namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/472 na JIN SHENG 1 yenye namba ya leseni
TZ/DSFA/EEZ/473.
Naye
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Yohana Budeba amewataka
wawekezaji kwenye bahari ya Tanzania kuwa waaminifu na kuzingatia
masharti na taratibu za kisheria ili nchi na wawekezaji waweze
kunufaika.
“Taratibu
zipo wazi ni muhimu kuzinangatia sheria namna nyingine tutaendelea
kusimamia sheria za nchi yetu kwa faida ya sasa na vizazi vya baadaye”
Alisisitiza Dkt. Budeba
Amesema
hatua iliyochukuliwa na Serikali ya kuzipiga faini meli hizo ni somo
kwa meli nyingine na kwamba Serikali itaendelea kuchukua hatua kali kwa
yoyote atakayebainika kutenda makosa ya uvuvi haramu katika bahari na
maziwani.
Aidha
amesema Serikali ipo tayari kufanya biashara na mtu yoyote ambaye
atazingatia masharti ya nchi, na kwamba taifa linajipanga ili kuwa na
makampuni yake ya TAFICO na ZAFICO yatakayoshuhulika na uvuvi ili
kunufaika na raslimali za uvuvi kama ambavyo inafanyika katika nchi
mbalimbali duniani.
Amesema hatua hiyo itasaidia kukuza ajira kwa wananchi, uchumi wan chi na kuanzisha viwanda vya kuchakata samaki na mazao yake.
Aliwashukuru
wadau wote wanaoshiriki kwenye mapambano ya uvuvi ambapo kipekee
alilishukuru shirika lisilo la kiselikali la Sea worrior kwa kutoa
mchango mkubwa kwenye operesheni Jodari ambayo imefanywa na wadau
mbalimbali nchini.
Post a Comment
karibu kwa maoni