0
Mama kadadaa jina maarufu la uigizaji anependa kuchukua uhusika wa mama wa Familia katika kuigiza ametaka wasanii wa tasnia ya Filamu kupendana na kuacha majungu ili waweze kuendelea mbele na kupata mafanikio.
Ameyazungumza hayo akizungumza na JOHN WALTER BLOG kuhusu filamu mpya inayotarajiwa kuja sokoni siku za usoni inayojulikana kwa jina la Ndoto yangu.
Mbali na hiyo Mama kadadaa alishafanya kazi nyingi akishirikiana na wasanii wadogo na wakubwa wenye majina kama mzee Jengua.
Mama huyu ambaye ni mama mzazi wa msanii wa Bongo Fleva Sha Boy aliewahi kutamba na nyimbo kama Naimani na zingine amesema mpango wake ni kufika mbali katika tasnia ya Filamu na kumtaja anaemkubali sana ni pamoja na Rihama Ali.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top