0
Mlima Ol Doinyo Lengai karibu na kijiji cha Ngare Sero, Mkoa wa Arusha. 
Mkoa wa Arusha ni moja kati ya mikoa 30 ya Tanzania. Imepakana na Kenya upande wa kaskazini. Mikoa ya jirani ni kufuatana na mwendo wa saa: Kilimanjaro, Manyara, Shinyanga na Mara. Mkoa wa Arusha ni Mkoa wa pili kwa Utajiri nchini Tanzania.
Wilaya zake ni Monduli, Longido, Meru, Arusha Vijijini, Arusha Mjini,Ngorongoro na Karatu. Makao makuu yapo Arusha mjini.
Eneo lake ni km za mraba 86,100 zikiwemo km² 2,460 za maji. Kati ya milima yake Oldoinyo Lengai (2,878 m) bado ni volkeno hai, na mlima Meru ni volkeno ya kulala tangu mw. 1910. Mvua hunyesha kati ya millimita 1,800 mm kwa mwaka mlimani Arusha hadi 508 mm kwa mwaka katika maeneo makavu.
Mkoa wa Arusha ndio kitovu cha utalii Tanzania Bara. Barabara ya lami Dar Es Salaam-Nairobi inavuka eneo lake. Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Kilimanjaro wahudumia miji ya Arusha na Moshi. Kuna mbuga za taifa na hifadhi za wanyamapori Ngorongoro, Serengeti, Olduvai, Arusha, Tarangire na Ziwa Manyara. Hifadhi ya Mlima Kilimajaro iko karibu.
Arusha hulimwa kahawa, nafaka, pareto, katani, pamba, alizeti. Fosfati inachimbuliwa Minjingu Mkoani Arusha, na takribani tani 48,000 kwa mwaka hutumiwa katika uzalishaji wa mbolea.
Kati ya wakazi wa mkoa kiasili ndio Waarusha, Wameru, Wairaqw na Wamassai.

Majimbo ya bunge

Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:
  • Arumeru Magharibi : mbunge ni Gibson Ole Mesiyeki (Chadema)
  • Arumeru Mashariki : mbunge ni Joshua Nassari (Chadema)
  • Arusha Mjini :mbunge ni Godbless Lema (Chadema)
  • Karatu : mbunge ni Wille Qulwi Qambalo (Chadema)
  • Longido : mbunge ni Onesmo Ole Nangole (Chadema)
  • Monduli : mbunge ni Kalanga Julius Laizer (Chadema)
  • Ngorongoro : mbunge ni William Tate ole Nasha (CCM)


Wilaya za Mkoa wa Arusha
Wilaya
Wakazi (2012)
Eneo km²
Arusha mjini
1,694,310
93 km²
Arusha vijijini
323,198
1,447 km²
Karatu
230,166
3,300 km²
Longido
123,153
7,782 km²
Meru
268,144
1,268 km²
Monduli
158,929
6,419 km²
Ngorongoro
174,278
14,036 km²
Jumla
1,288,088
34,526 km²
Marejeo: Mkoa wa Arusha



Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top