Licha ya elimu ya utunzaji wa mazingira na kutumia vyoo kutolewa kwa wananchi lakini bado imeonekana kuwa changamoto kubwa katika maeneo mengi hapa nchini.
Wako wengine wenye vyoo lakini matumizi yake sio mazuri,usafi haufanyiki na vingine havina ubora.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira LUHAGA MPINA.
Akitoa taarifa kwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira LUHAGA MPINA ambaye amefanya ziara mkoani MANYARA, Mkuu wa wilaya ya BABATI , RAYMOND MUSHI amesema kuwa ni asilimia 57 tu ya wakazi wa mkoa huo ndio wenye vyoo.
Kufuatia hali hiyo, Naibu Waziri MPINA ametoa muda wa miezi mitatu kwa uongozi wa mkoa wa MANYARA kuhakikisha Wakazi wote wa mkoa huo wanakuwa na vyoo.
Post a Comment
karibu kwa maoni