Mgogoro wa Maji umeibuka Katika Kijiji cha
OLIGILAI Kata ya KIUTU Wilayani ARUMERU baada ya Mamlaka ya Maji safi na
Taka kujengea chanzo cha maji na kuweka mashine ya kusukuma maji
Mgogoro wa Maji umeibuka Katika Kijiji cha OLIGILAI Kata ya
KIUTU Wilayani ARUMERU baada ya Mamlaka ya Maji safi na Taka kujengea
chanzo cha maji na kuweka mashine ya kusukuma maji kupeleka katika
matanki yao bila idhini ya Wananchi hao,huku wakiwatuhumu Viongozi kuuza
chanzo hicho kinyemela.Hayo yamejitokeza kwenye Mkutano Mkuu wa Kijiji cha OLIGILAI ambapo wananchi walipaza sauti kuwa Mamlaka hiyo ya Maji imechukuwa chanzo hicho bila kuwashirikisha na kukiingiza katika Matenki ya kukusanyia Maji na kuyapeleka Jijini ARUSHA wakati wao hawana maji wala Kijiji hakipewi malipo yeyote.
Kufuatia mvutano huo ambao ulitishia kuvunjika kwa Mkutano Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Maji Safi na Taka wa Jijini ARUSHA AUWSA RICHARD LAIZER amewaahidi Wananchi hao kuwa ndani ya siku Tatu watarudisha chanzo hicho baada ya kujadiliana na Mkurugenzi wake.
Kijiji cha OLIGILAI ndipo mahali ambapo Mamlaka ya Maji inavyanzo vingi wa Maji ilivyo vijengea kwa kukusanya maji ya usambaza Jijini ARUSHA na Viunga vyake.
Post a Comment
karibu kwa maoni