Mbunge wa jimbo la Babati mjini [CHADEMA]Mheshimiwa Pauline philip Gekul amenusurika kifo baada ya gari lake kuacha njia na kupinduka katika mtaa wa Nangara ziwani Mjini Babati.
Gekuli alikuwepo katika msafara wa naibu waziri wa Mazingira Luaga Mpina aaliepo wilayani hapa katika ziara yake ya kikazi inayokamilika kesho.
Kwa upande wa mashuhuda walioshuhudia tukio hilo wanasema gari hilo limepinduka wakati dereva alipokuwa akijaribu kumkwepa dereva boda boda aliekuwa kati kati ya bara bara.
Dereva aliekuwa akimwendesha Mbunge anasema alimpigia honi lakini hakupisha ndipo katika harakati za kumkwepa gari likaacha njia"alisema dereva huyo.
Katika msafara wa naibu waziri gari la mheshimiwa Gekul liliachwa nyuma.
Hata hivyo Naibu waziri wa Mazingira Luaga Mpina aliekuwa akielekea kukitembelea kiwanda cha Sukari Manyara Sugar amehairisha ziara hiyo kutokana na tukio hilo.
Naibu waziri alimtembelea Gekul kumjulia hali akiwa na Mbunge wa Babati vijijini mheshimiwa Jituson.
Viongozi mbalimbali wa Chadema Babati wamefika kumjulia hali mheshimiwa Mbunge katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Manyara.
Gekuli alikuwepo katika msafara wa naibu waziri wa Mazingira Luaga Mpina aaliepo wilayani hapa katika ziara yake ya kikazi inayokamilika kesho.
Kwa upande wa mashuhuda walioshuhudia tukio hilo wanasema gari hilo limepinduka wakati dereva alipokuwa akijaribu kumkwepa dereva boda boda aliekuwa kati kati ya bara bara.
Dereva aliekuwa akimwendesha Mbunge anasema alimpigia honi lakini hakupisha ndipo katika harakati za kumkwepa gari likaacha njia"alisema dereva huyo.
Katika msafara wa naibu waziri gari la mheshimiwa Gekul liliachwa nyuma.
Hata hivyo Naibu waziri wa Mazingira Luaga Mpina aliekuwa akielekea kukitembelea kiwanda cha Sukari Manyara Sugar amehairisha ziara hiyo kutokana na tukio hilo.
Viongozi mbalimbali wa Chadema Babati wamefika kumjulia hali mheshimiwa Mbunge katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Manyara.
Post a Comment
karibu kwa maoni