Matukio
ya Madiwani kuhama Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na
kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) yamezidi kushika kasi, baada ya
diwani wa tano wa Kata ya Olsunyai, Elirehema Nnko, kuhama chama hicho
jana.
Aidha, tangu kuanza kwa matukio ya kujiuzulu madiwani wa chama hicho mwaka jana, hadi sasa wamefika watano walioachia ngazi.
Madiwani
wa Chadema waliojiuzulu na na kjiunga CCM ni Credo Kifukwe (Muriet),
Geyson Ngowi (Komandolu), ambao tayari kaza zao uchaguzi umesharudiwa na
CCM kuzinyakua.
Wengine
ambao wamejiuzulu karibuni na uchaguzi bado kufanyika ni Elirehema Nnko
(Olsunyai), Prosper Msofe (Daraja Mbili) na Obeid Meng'oriki wa Kata
ya Terati.
Akizungumza
jana wakati akitangaza kuachia ngazi Chadema na kujiunga CCM, Elirehema
alisema sababu kubwa ya kuhama ni za kibiashara.
“Biashara zangu haziendi vizuri nadhani nikiwa CCM zitabadilika natakuwa nzuri,”alisema.
Sababu
hiyo aliyotoa diwani huyo inakuwa tofauti na walizotoa wenzake
waliomtangulia kutoka chama hicho ambao wanadai sababu kubwa ni kuguswa
na jitihada za Rais John Magufuli na kuamua kumuunga mkono kwa kujiunga
na chama tawala.
Post a Comment
karibu kwa maoni