Hali ya mbunge wa Babati mjini Paulina Gekul [CHADEMA]inaendelea kuimarika baada ya kupata ajali ya gari akiwa kwenye ziara ya naibu waziri wa Muungano na Mazingira Luhaga Mpina.
Ajali hiyo
ilitokea jumamosi ya wiki iliyopita [24.2.2017] baada ya gari la mbunge lenye
namba za usajili T 189 BHQ kuacha njia na kupinduka katika mtaa wa Nangara ziwani mjini Babati bara
bara ya kuelekea Dodoma.
Baada ya ajali hii kutokea mmbunge Paulina Gekul ambaye
ni mmbunge wa babati mjini alikimbizwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa
manyara na kulazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi I.C.U na baadaye taarifa
ilizozipata blog hii ni kwamba alihamishiwa katika hospitali ya KCMC Moshi kwa
uchunguzi zaidi.
Hata hivyo baada ya ajali kutokea naibu waziri wa
mazingira alilazimika kuahirisha ziara yake ya kutembelea maeneo mbalimbali
ndani ya mji wa babati huku mpina akiipongeza halmasahauri ya mji wa babati kwa
kutambua umuhimu wa kutunza mazingira katika hali ya usafi baada ya kununua
gari kwaajili ya kubebea taka lenye thamani ya zaidi ya milioni 200.
Naibu waziri
alikuwa katika ziara yake ya kikazi kwa siku mbili katika mji wa Babati
akitembelea maeneo mbalimbali,alikitembelea kiwanda cha Perfume SIERA,Eneo la
Dampo Sigino,Ziwa Babati na kujionea gari la taka la kisasa lililonunuliwa kwa
pesa za Halmashauri lenye thamani ya shilingi milioni 230.
Post a Comment
karibu kwa maoni