MKUU
wa Shule ya Sekondari Tumuli katika Wilaya ya Mkalama, mkoani Singida,
Richard Makala (58) amejinyonga kwa kamba kutokana na kile
kinachodhaniwa kuelemewa na upweke.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Debora Magiligimba, amesema mjini Singida kuwa, Makala alijinyonga jana saa 1 asubuhi.
Ameeleza
kuwa Makala alikutwa amejinyonga kwa kutumia kamba iliyotengenezwa kwa
vipande vya chandarua iliyofungwa juu ya mti umbali wa mita 130 kutoka
nyumbani kwake.
Amesema,
chanzo cha tukio hilo hakijajulikana na kwamba hakuna mtu au watu
wanaoshikiliwa kutokana na tukio hilo na kuongeza kuwa polisi inaendelea
na upelelezi kubaini kilichomsibu mwalimu huyo.
Hata
hivyo, Mjumbe wa Bodi ya shule hiyo, Mabruki Ng’ui ameliambia gazeti
hili jana kuwa mwalimu huyo alikuwa anaishi peke yake kwa muda mrefu
baada ya mkewe ambaye ni Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Tanzania Tanzania (KKKT) Kitusha wilayani Iramba kuamua kutengana naye
kutokana na unywaji pombe.
"Huyu
bwana amekuwa kwenye ndoa ya jina tu maana mke wake amekuwa akiishi
mbali naye kwa kipindi kirefu sana, amekuwa mpweke kwa muda mrefu mno
huenda hicho ndicho kilichosababisha ajitoe roho yake," amesema Mjumbe
huyo wa Bodi.
Makala ni mzaliwa wa kijiji cha Ndago, wilayani Iramba na anatarajiwa kuzikwa leo nyumbani kwake.
Ameacha mjane na watoto watano.
Post a Comment
karibu kwa maoni