0
Butiama. Serikali imesitisha shughuli za kuchimba madini ya dhahabu katika migodi ya Buhemba na kuagiza Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), kulinda eneo hilo hadi Kampuni ya Taifa ya Madini (Stamico), itakapokamilisha uchunguzi wa usalama kwenye eneo hilo.

Amri hiyo ilitolewa  Mkuu wa Mkoa wa Mara, Dk Charles Mlingwa baada ya kutokea ajali ya pili katika migodi hiyo na kusababisha vifo vya wachimbaji wadogo wanne na huku wengine sita wakijeruhiwa.

Amesema Serikali imefikia uamuzi huo ili kuepuka uwezekano matukio mengine ya ajali kutokea na kuendelea kugharimu maisha ya wachimbaji wadogo wanaofanya shughuli zao katika eneo hilo.

Usiku wa kuamkia Februari 13, mwaka huu, mgodi mwingine uliporomoka eneo hilo na kusababisha vifo vya watu watatu huku 15 wakijeruhiwa.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top