0
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi WILLIAM LUKUVI 
 
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi WILLIAM LUKUVI amekutana na uongozi wa mikoa ya TANGA na MANYARA lengo likiwa ni kumaliza mgogoro wa ardhi uliodumu kwa zaidi ya miaka kumi baina ya wananchi wa wilaya ya KILINDI mkoani TANGA  na KITETO mkoani MANYARA.

Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigel akizungumza katika mkutano huo.
Waziri LUKUVI amesema wakati sasa umefika wa kumaliza tatizo hilo hivyo kuwaomba viongozi wa mikoa yote miwili kutoa ushirikiano kwa wataalamu watakaokwenda kuweka kuhakiki alama za mpaka.

Mkuu wa mkoa wa Manyara Dk. Joel Bendera akizungumza katika mkutano huo.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Tanga MARTINE SHIGELA amesema watahakikisha wanajipanga vizuri katika kutoa ushirikiano kwa wataamu wa ardhi.

Naye mkuu wa mkoa wa Manyara JOEL BENDERA amewataka viongozi walioshiriki kwenye kikao hicho kutobadili makubaliano ya awali ili waweze kufikia lengo.
Katika kumaliza mgogoro huo serikali haitaweka mpaka mpya bali itazingatia tangazo la gazeti la serikali namba 95 la mwaka 1961.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top