Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionesha mfuko wa kubebea mbolea ya
kiwanda cha Minjingu mkoani Manyara wenye maandishi yanayoonesha kuwa
mbolea hiyo imetengenezwa nchini Kenya. Jambo hilo lilimkera sana Waziri
Mkuu na aliuagiza uongozi wa kiwanda hicho kuandika barua ya
kumuaomba radhi Rais John Pombe Magufuli kwa kitendo hicho. Kushoto
ni Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt, Charles Tizeba na wapili
kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dkt. Joel Bendera.(Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha mfuko wa kubebea mbolea ya kiwanda
cha Minjingu mkoani Manyara wenye maandishi yanayoonesha kuwa mbolea
hiyo imetengenezwa nchini Kenya. Jambo hilo lilimkera sana Waziri Mkuu
na aliuagiza uongozi wa kiwanda hicho kuandika barua ya kumuaomba radhi
Rais John Pombe Magufuli kwa kitendo hicho. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu).
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema haridhiki na hali aliyoikuta kwenye
kiwanda cha kutengeneza mbolea cha Minjingu baada ya kubaini kuwa
wanatumia mifuko yenye lebo ya Kenya wakati mbolea hiyo inazalishwa hapa
nchini.
Kutokana
na hilo, Waziri Mkuu amewataka wamiliki wa kiwanda hicho waandike barua
kwa Mheshimiwa Rais Dk. John Pombe Magufuli kabla hajamaliza ziara yake
Jumatano, Februari 22, 2017 apate nakala ya barua hiyo.
Ametoa
agizo hilo leo (Jumapili, Februari 19, 2017) baada ya kutembelea
kiwanda hicho kilichopo wilaya Babati akiwa katika siku ya tatu ya ziara
yake mkoani Manyara. Waziri Mkuu amerejea Babati leo akitokea Dar es
Salaam ambako alikuwa na ratiba za kitaifa.
“Nilikuja
kukagua kiwanda baada ya kupokea malalamiko kuwa mbolea hii haikubaliki
huko vijijini. Watafiti wameonyesha kuwa ikitumika inasaidia kutoa
mazao mengi. Lakini wakati niko kiwandani nimekerwa kukuta mifuko ya
kupakia mbolea hii ina anuani ya Nairobi, Kenya wakati mali ghafi
inatoka Tanzania,” amesema.
“Ni
kwa nini mifuko hii ina anuani ya Kenya? Hapa tulipaswa tuone anuani ya
Babati! Je mlipata kibali kutoka serikalini? Tena kuna lebo ya TBS. Kwa
nini Tanzania haionekani? Kwani malighafi iko Kenya? Haiwezekani, ni
lazima uandike barua na uombe radhi kwa Mheshimiwa Rais Magufuli. Yeye
anahimiza ujenzi wa viwanda ndani ya nchi, halafu ninyi mnafanya hivyo?”
Akiwa
ndani ya kiwanda hicho, Waziri Mkuu alikuta baadhi ya mifuko ya mbolea
ikiwa imeandikwa: ‘County Government of Bungoma’, ina nembo ya Serikali
ya Kenya, na anuani ikionesha kuwa mbolea hiyo imetengenezwa na kiwanda
cha mbolea cha Minjingu lakini anuani inasomeka P. O Box 2941 – 00200
Nairobi, Kenbro Industrial Park, Mombasa Road; namba ya simu
+254-20-6000-970 lakini mifuko hiyo pia ina muhuri wa TBS.
Baadhi ya mifuko ilikuwa ikipakiwa ndani ya lori tayari kwa kusafirishwa kwenda kwa wateja.
Pia
amesema atamwagiza Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw.
Charles Mwijage aje hapa na wanasheria wake na wataalamu kutoka Tume ya
Ushindani wa Kibiashara (FCC) ili waje kuangalia hatua gani zinapaswa
kuchukuliwa.
“Kwa
staili hii hii tumeona watu wakinunua kahawa yetu na kwenda kuipakia
upya huku wakiweka lebo za kwao. Leo hii hata Tanzanite pia inasemwa
imetengenzwa India. Hatuwezi kukubali hali hii iendelee,” amesisitiza.
“Tukiruhusu
hali hii, watu watajuaje kuwa mbolea hii ambayo ni first class duniani
kuwa inapatikana Tanzania? Kiwanda chetu, ardhi yetu, suala la kutangaza
nchi yetu kwa kutumia bidhaa zetu litafanikiwa kwa njia hii kweli?”
“Nataka
wakati namaliza ziara nipate taarifa ya hili jambo pamoja na nakala ya
barua ambayo imetumwa kwa Mheshimiwa Rais,” amesisitiza.
Akitoa
maelezo kuhusu hali hiyo, Mkurugenzi wa kiwanda hicho, Bw. Tosky Hans
alimweleza Waziri Mkuu kwamba wametumia lebo hiyo kutokana na
makubaliano na wanunuzi jibu ambalo Waziri Mkuu hakulikubali na
kusisitiza kuwa anapaswa aombe radhi.
Waziri
Mkuu kesho anaendelea na ziara yake wilayani Mbulu ambako atatembelea
hospitali ya Haydom, kuzungumza na watumishi wa wilaya hiyo na kuzindua
shule ya sekondari Singland.
Post a Comment
karibu kwa maoni