Chama
cha Demokrasia na Maendeleo kunatarajia kuwakaribisha wanachama wapya
waliojiunga leo na chama hicho akiwamo msanii maarufu nchini wa fani ya
uigizaji wa filamu, Wema Sepetu (28).
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilianio wa Chadema, Tumaini Makene amesema leo (Alhamisi) kuwa chama hicho kupitia Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe, baada ya kesi ya kikatiba namba 1 ya mwaka 2017 inayotarajiwa kuwasilishwa Mahakama Kuu leo, kitazungumza kwa umma kupitia waandishi wa habari kuwakaribisha wanachama wapya waliojiunga leo akiwemo Wema Sepetu.
Wema
pamoja mama yake, leo aliongozana na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman
Mbowe pamoja na viongozi wengine wa chama hicho kwenye mahakama kuu
jijini Dar es Salaam.
Msanii huyo aliyeshinda taji la Miss Tanzania mwaka 2006, alikuwa kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kabla ya kuhamia Chadema.
Post a Comment
karibu kwa maoni