Benny Mwaipaja,
WFM, Tunduma
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, akiwa na Mgeni wake ambaye ni Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika Bw. Makhtar Diop, wakiwa katika chumba cha kupumzikia wageni maalumu katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam. Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Burundi, Somalia na Malawi Bi. Bella Bird. |
Kituo hicho
kimeanza kufanyakazi tangu Februari mosi mwaka huu, ambapo watumiaji wa mpaka
huo watakuwa wakihudumiwa upande mmoja wa mpaka badala ya utaratibu uliokuwa
ukitumika awali ambapo watumiaji walilazimika kukaguliwa mizigo yao kila upande
hatua iliyokuwa ikichelewesha biashara katika mpaka huo
Naibu Katibu Mkuu
wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban, Katibu Mkuu Wizara ya
Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda na Naibu Waziri wa mambo ya
Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba Yahya, wameeleza kuridhishwa na kazi
inayofanyika mpakani hapo kupitia mfumo huo mpya.
Hata hivyo baadhi
ya madereva wanaosafirisha bidhaa kupitia mpaka huo wa Tunduma na Nakonde,
pamoja na kupongeza utaratibu huo mpya, wameiomba Serikali iwasiliane na upande
wa Zambia, ili waongeze kasi ya kuruhusu malori kuendelea na safari yanapofika
mpakani hapo bila kucheleweshwa ili kwenda sambamba na kasi ya upande wa
Tanzania, ambao umeboresha kwa kiwango kikubwa utoaji wa huduma.
Katibu Mkuu wa
Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda, amesema kuwa
makubaliano yaliyofikiwa kati ya Serikali na watoa huduma katika mpaka huo
yalikuwa ni kuwahudumia wadau wanaotumia mpaka huo kwa muda usiozidi siku moja
na kuwataka madereva wa malori wanaokwazwa kuwasiliana na mamlaka zinazohusika.
Prof. Mkenda
amewaonya mawakala wa Forodha katika mipaka yote nchini watakao bainika kwa
namna moja au nyingine kuwachelewesha wenye malori kwa makusudi watafutiwa
leseni zao za kufanya biashara hiyo
“Tunataka mpaka
huu wa Tunduma na Nakonde ufanye kazi kwa ufanisi na ubora wa hali ya juu ili
kuiwezesha bandari yetu ya Dar es Salaam kufanyakazi kwa kiwango cha juu ili
kukuza biashara nchini” Alisisitiza Prof. Mkenda
Amesema kuwa
Serikali imeunda timu ya wataalam wanaopitia kero mbalimbali za mazingira ya
ufanyaji biashara na uwekezaji hapa nchini, itakayo peleka mapendekezo namna ya
kuboresha mazingira hayo kwa kuwa mchango wa sekta binafsi wakiwemo wawekezaji,
unatambuliwa na Serikali
Kwa upande wao, Afisa
Mfawidhi wa Forodha , Idara ya Forodha na Ushuru wa Bidhaa-Tunduma, Bw. Magori
Magori, na Mbunge wa Jimbo la Tunduma, Frank Mwakajoka, wameelezea kukithiri
kwa vitendo vya magendo mpakani na kero ya vizuizi lukuki kwenye njia kuu ya
Dar es salaam hadi Tunduma, hatua inayokwaza biashara kati ya Tanzania na
Zambia.
Kwa upande wake
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban,
ameiagiza Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kuchunguza na kuishauri Serikali namna ya
kuboresha matumizi ya pesa ya Zambia (kwacha) ili kupunguza changamoto ya
ufanyaji holela wa biashara ya kubadilisha fedha hiyo katika mpaka wa
Tunduma/Nakonde upande wa Tanzania na Zambia na mpaka wa Kasumulu/Songwe,
upande wa Tanzania na Malawi.
Maagizo hayo
yanafuatia kuwepo kwa biashara holela ya ubadilishaji fedha hiyo mpakani huku
Benki Kuu ikieleza kuwa fedha hizo (kwacha) haziko kwenye orodha ya fedha za
kigeni zinazotambulika rasmi hapa nchini hivyo kuwa vigumu kudhibiti mwenendo
wake.
Naye Naibu Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba Yahya, ameahidi kuwa
wizara yeke itaifanyia kazi changamoto ya uwepo wa vizuizi vingi vya malori
yaendayo masafa marefu kwakuwa vinasababisha adha isiyo ya lazima na kukwamisha
biashara nje ya nchi.
“Kwa kuwa malori
mengi yaendayo masafa marefu kutoka Bandari ya Dar es Salaam yanafungwa vifaa
maalumu vya ufuatiliaji mwenendo wake, hakuna sababu ya trafiki kuyasimamisha
kila wakati, tunataka lori likikaguliwa Dar es Salaam lisafiri bila
kusimamishwa hadi litakapofika mpakani ambapo litafanyiwa ukaguzi wa mwisho”
aliongeza Balozi Yahya.
Kuanza kufanyakazi
kwa kituo cha pamoja cha Forodha cha mpaka wa Tunduma/Nakonde kunafuatia
maagizo yaliyotolewa na Marais Dkt. John Pombe Magufuli na Edgar Lungu wa
Zambia, alipofanya ziara ya kikazi nchini Tanzania hivi karibuni ili
kurahisisha biashara katika ya nchi hizo nan chi wanachama wa Jumuiya ya
Madola-SADC, na kama mambo yatabaki kama yalivyopangwa, kitazinduliwa rasmi na Mawaziri
wa kisekta mwezi Machi, mwaka huu.
Post a Comment
karibu kwa maoni