0
Baadi ya Wazee wa kijiji cha Sigino wamehusisha ajali zinazotokea mara kwa mara kona ya Logia Babati MANYARA na imani za kishirikiana.
Wakizungumzia eneo hilo wazee hao wameeleza kuwa kuna milio isiyoeleweka inasikika katika eneo hilo huku wakihisi harufu za marashi na haonekani mtu.
Mmoja wa wazee hao ameongeza kuwa huwa jogoo anawika na ndama kulia na hakuna nyumba jirani na eneo hilo jambo linalowaacha Dailema.
Hayo yamejiri baada ya kutokea ajali jana jioni \ambapo gari la mizigo lililokuwa limebeba Mashudu likitokea Shinyanga kwenda Arusha liliacha njia na kuzama katika bonde kona ya Logia na kuharibika vibaya.
Hakuna alieripotiwa kupoteza maisha katika ajali hiyo.
PICHA HIZI HAPA.
Hata hivyo walioshuhudia ajali hiyo wanaseama kuwa dereva na utingo wake wamlitoka salama na kuchukua vitu vyao na kuondoka na haijulikani walipoelekea mpaka sasa.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top