0
Muimbaji wa Bongo Fleva na muigizaji wa filamu Dafroza Rober 'Apple' ameingia katika mzozo mkubwa na mwenzake Ashura 'A.Stanza' baada ya kurushiana maneno huku A Stanza akidai kuwa Apple ni ni Mshirikina.
Apple D akizungumzia hilo katika kipindi cha Mseto, redio Manyara Fm kinachoruka hewani jumatatu mpaka alhamisi majira ya saa nne asubuhi mpaka saa saba  amesema kuwa amechukizwa na kauli za stanza anazozitoa kwa watu mitaani kuwa yeye ni mchawi huku akisema kuwa hiyo inamchafulia jina lake.
Amesema hayupo tayari kuchafuliwa jina lake na kwamba   mashabiki wake wapuuze maneno hayo wanayoyasikia mitaani.
Kwa upande wake A stanza amekiri kusema maneno hayo akisema ameamua kuyasema hayo kutokana na kukerwa na tabia zake za kutembea na waume za watu akiwemo  mpenzi wake ambaye ni Producer Mr.Perfume.
Akijibu hilo Apple amekana kutembea na Producer huyo kutoka maisaka Record na hawezi kufanya hivo.TAZAMA VIDEO HAPA AKAIZUNGUMZA APPLE D NA  NAI NAI  PAMOJA NA HQ KATIKA KIPINDI CHA MSETO MANYARA FM


Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top