0
Mama Amina Mkadingile mkazi wa kijiji cha Likonde wilaya ya Mtwara vijijini  ameomba watanzania kumsaidia matibabu ya mtoto wake Mwanaidi Hamisi wa darasa la tano aliyepata ulemavu wa mikono baada ya kuungua moto akiwa shuleni,tukio lililopolekea mume wake kumkimbia kukwepa majukumu ya kuuguza mtoto huyo.

Akiongoea kwa uchungu mama Amina Mkadengile anasema mtoto wake mwanaidi alipata ulemavu huo akiwa shuleni baada ya kusukumwa na mwenzake kwenye shimo la kuchomea taka katika shule ya msingi likonde  na hivyo kuungua vibaya mikono yake miwili, na hivyo kusaidiwa matibabu ya mkono mmoja na Ofisi ya elimu mkoa wa Mtwara, huku mkono wa pili ukiwa bado unaitaji matibabu.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha Likonde amekiri mama Mkandengile kuhangaikia matibabu ya mtoto wake pekee,hali iliyolazimu chama cha msaada wa kisheria kwa wanawake na watoto mkoani Mtwara Paraligo kumsaidia mama huyo kupata haki zake.

Matibabu ya mkono wa pili yanahitaji gharama ya shilingi milioni moja huku akitoa namba zake za simu kwa mtu atakayewiwa kumsaidia ambazo ni 0787894070

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top