0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli, leo March 29 2017 ameteua kamati ya wataalamu watakaofanya uchunguzi kwa lengo la kubaini kiwango cha madini kilichomo katika makontena yenye mchanga wa madini yanayoshikiliwa katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa kamati hiyo yenye wajumbe 8, inatakiwa kuanza kazi haraka iwezekanavyo.
Wajumbe wa Kamati hiyo ni;
⦁ Prof. Abdulrahman Hamis Mruma
⦁ Prof. Justianian Rwezaura Ikingula 
⦁ Prof. Joseph Bushweshaiga 
⦁ Dkt. Yusuf Ngenya
⦁ Dkt. Joseph Yoweza Philip
⦁ Dkt. Ambrose Itika 
⦁ Mohamed Zengo Makongoro
⦁ Hery Issa Gombela
Wajumbe wote wa kamati hii wanatakiwa kufika ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi, Ikulu Jijini Dar es Salaam Ijumaa tarehe 31 Machi, 2017 saa 4:00 asubuhi.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top