0
Image result for AFISA UHAMIAJI MANYARA PETER KUNDY
Idara ya uhamiaji mkoa wa Manyara inawaomba wananchi wakiwemo wamiliki wa vyombo vya usafiri,nyumba za kulala wageni popote pale walipo watoe taarifa wanapoona watu wanaowatlia mashaka.
Idara hiyo inawasihi waajiri kwenye sekta mbalimbali kama viwanda,mashamba,utalii,biashara na taasisi nyinginezo kuhakikisha kuwa raia wa kigeni watakao waajiri wanakuwa na vibali vya ukaazi nchini.
Msemaji wa idara ya uhamiaji mkoa wa Manyara afisa uhamiaji Peter J.Kundy amewataka wananchi  wajitoe bila woga kwa kufanya hivyo watakuwa wanashiriki kutunza usalama wa mkoa wao na taifa kwa ujumla.
Katika hatu nyingine, Idara ya uhamiaji mkoa wa Manyara imetoa taarifa za utendaji kazi wake kwa kipindi cha mwezi January 2016 mpaka  Februari 2017.
Akitoa taarifa hiyo kwa Umma Kamishna wa uhamiaji [Afisa uhamiaji mkoa wa Manyara] Peter J.Kundy ameeleza huduma zilizotolewa na idara hiyo kwa kipindi cha January -Disemba 2016 ni utoaji wa pasipoti na Hati nyingine za safari ambapo jumla ya maombi ya pasipoti za kawaida [Ordinary Passport] mia mbili na arobaini na saba [247] yaliyopokelewa pamoja hati za safari za dharura (Emegency Travel Document)mia tisa themanini (980)zimetolewa.
Kuhusu vibali vya ukaazi na hati za ufuasi Kundy amesema kuwa jumla ya maombi ya vibali vya kuishi nchini thelathini (30) vilitolewa kwa mchanganuo ufuatao;Daraja "A"-2,daraja "B"-01,daraja "C"-25 na hati za ufuasi mbili (02).
Aidha ameeleza kuwa Maombi ya uraia wa Tanzania yalipokelewa matatu (03) na kushughulikiwa.
Afisa huyo amesema kuwa wameendesha doria,Kaguzi na  misako na kukamatwa watu mia mbili arobaini (240) katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Manyara walikamatwa na kufanyiwa mahojiano  ambapo waliothibitishwa uhalali wa uraia wao na vibali vyao vya kuishi hapa nchini ni 173,walioshtakiwa na kufikishwa mahakamani ni 37,waliofungwa\kulipa faini 34,walioondoshwa nchini watatu (3) raia wa Kenya mmoja na kutoka nchini Malawi wawili huku wahamiaji walowezi 30 wakiwa wanasubiri hatua zaidi.
Pia amesema wamekuwa wakitoa elimu ya uhamiaji shirikishi kwa vijana wanaochukua mafunzo ya uaskari mgambo na kwa wananchi kwa ujumla kwa lengo la kuwawezesha raia na wageni wafahamu kikamilifu taratibu za ukaazi na sheria nyingine za uhamiaji na wajibu wao katika suala zima la ulinzi wa mkoa dhidi ya wahamiaji haramu na wageni wasiofuata sheria za uhamiaji.
Akielezea mafanikio amesema"Kwa kipindi chote hicho ofisi ya uhamiaji imepata mafanikio ikiwa ni pamoja na miasko,dori na ukaguzi iliyofanikiwa kukamata wahamiaji 240,tumefanikiwa kuongeza ukusanyaji wa Mdhuli ya serikali kutoka shilingi 20,495,000/-kwa mwaka 2015 hadi shilingi 22,100,000/-kwa mwaka 2016".
"Tumefanikiwa kutoa elimu ya uhamiaji shirikishi kupitia mafunzo ya mgambo katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Manyara na baadhi ya watendaji wa kata na vijiji".alisema Kundy.
Lakini pia amesema kwa kushirikiana na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU)mkoa wa Manyara idara ya uhamiaji mkoa wa Manyara imefanikiwa kutoa mafunzo ya maadili kwa watumishi,kuzuia na kupoambana na rushwa kwa watumishi wake.
Amesema pamoja na mafanikio hayo zipo changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku akizitaja changamoto hizo amesema mojawapo ni ushiriki mdogo/hafifu wa raia katika kutoa taarifa zinazowezesha jeshi la uhamiaji na vyombo vingine vya usalama kufanya kazi kwa ufanisi zaidi akitolea mfano kuwaripoti wageni wasiofuata sheria na taratibu za uhamiaji.
Amesema matarajio yao kwa Mwaka huu wa 2017 ni kutoa huduma kwa weledi,ubora wa kujali muda kuendana na mkataba wa huduma kwa wateja wa idara (immigration client services charter),Kuongeza doria,misako na kaguzi katika kuwabaini wahamiaji haramu na watu wanaokiuka sheria na taratibu za uhamiaji,Kuongeza kasi ya ukusanyaji na udhibiti wa madhuli ya serikali sambamba na kutoa elimu ya uhamiaji shirikishi kwa makundi mbalimbali katika jamii yakiwemo mashuleni,taasisi za dini,wajasiriamali nk.
Idara ya uhamiaji ni moja kati ya vyombo vya ulinzi na usalama nchini na ipo chini ya wizara ya mambo ya nje ya nchi.Idara ya uhamiaji inatekeleza majukumu yake kwa kufuata katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania,sheria,kanuni na miongozo mbalimbali ya nchi.Sheria kuu zinazotumiwa na idara ya uhamiaji ni sheria ya uhamiaji sura ya 54brejeo la mmwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na sheria ya uhamiaji Na.8 ya mwaka 2015,sheria ya uraia sura ya 357 rejeo la mwaka 2002,na sheria ya pasipoti na hati za safari Na.20/2002.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top