0
Ali Kiba
Umahiri wa Msanii Ali kiba umeonekana kwa mashabiki wa mkoa wa Manyara baada ya kupiga kura  kumchagua kwa wingi katika mpambano uliomkutanisha na Diamond Plutnum.
Diamond Plutnum
 Kipindi cha Sartuday Box Jumamosi ya leo 4.3.2017 asubuhi katika kipengele cha nani mkali 92.1 Redio Manyara Fm mtangazaji wa kipindi akiwa JOHN WALTER a.k.a STOVE IRON aliruhusu simu pamoja na ujumbe mfupi wa maandishi ambapo katika kura 74 zilizopigwa na wasikilizaji zilikuwa jumla 74 kati ya hizo 60 zikaenda kwa King Kiba na 14 zikaenda kwa Diamond Plutnum Simba.
Mtangazaji wa kipindi John Walter.[STOVE IRON]
Kipindi hiki kinaruka kila Jumamosi na kupambanisha wasanii wanaofanya mziki wa aina moja na zinachezwa kete tatu za kila mmoja kisha msikilizaji ndio anamchagua anaye mkubali na kila anaepiga kura anaonyesha ni kwa kiasi gani wanamkubali wanaemchagua.
Mpambano huo ulirudiwa baada ya wiki iliyopita kukosekana mshindi kwani wote walipata kura 34-34 na mashabiki wakapendekeza mpambano huo urudiwe tena.
Wasanii hao wawili wanaofanya vizuri tangu walipoanza game wamezidikujizolea mashabiki kila kona ya dunia baada ya kuonyesha uwezo wao wanapokuwa jukwaani.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top