Jeshi la
polisi mkoa wa Manyara limekataza maandamano ya BLACK THURSDAY yaliyopangwa
kufanyika nchi nzima hii leo.
Akizungumza
na WALTER HABARI asubuhi leo Agust 31 Kamanda wa Polisi mkoa wa
Manyara Francis Masawe amesema kuwa hawajapata taarifa yeyote kuhusu maandamano
hayo hivyo hayatafanyika.
‘Hakutakuwa
na maandamano yeyote na endapo watafanya watakuwa wanatuchokoza’alisema Kamanda
Masawe.
Mwenyekiti
wa Baraza la vijana wa Chadema mkoa wa Manyara Frank Oleleshwa amesisitiza kuwa
watafanya maandamano hayo huku akiwataka vijana na wananchi wengine wajitokeze
kuwaunga mkono.
‘Mkoa wa
Manyara unaunga mkono kauli ya mwenyekiti wetu wa Taifa kwamba siku ya leo
tunaitangaza kama Lhamisi nyeusi kupinga polisi kukamata viongozi wetu ovyo’.
Aliongeza
kuwa wameshaliandikia jeshi la polisi barua na mpaka sasa bado hawajajibiwa ila
halitawazuia wao kufanya maandamano yao ya amani.
Wiki
iliyopita, baraza hilo la vijana lilitangaza kuwepo kwa maandamano ya amani
siku ya kesho ambayo waliyapa jina la “Black Thursday” yenye lengo la
kushinikiza kuwepo kwa haki za kisiasa, kiuchumi, utawala wa sheria pamoja na
haki za binadamu nchini.
Post a Comment
karibu kwa maoni