0

Jana  kulisambaa habari zisizokuwa za kweli kuhusu kifo cha Diwani wa kata ya Kijichi Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam, Tausi Milanzi.

Habari hizo ambazo zililikuwa zinasambaa kwa kasi  kwenye mitandao ya kijamii jambo lililopelekea Globu ya Jamii  kutafuta ukweli wa jambo hilo na kuwasiliana na watu wanaohusika.

Globu ya Jamii  ilimtafuta Diwani huyo kwa njia ya simu ya kiganjani na kuzungumza nae ambapo amekanusha uwepo wa taarifa hizo na kueleza kuwa yeye ni mzima wa afya na anaendelea na shughuli zake kama kawaida na kuwataka wananchi wake waendelee kumuunga mkono na kupuuza uvumi huo.

"Mimi mzima na shangaa hao amabo wamezusha kuwa mimi nimefariki Dunia hivyo wanatakiwa  kujua kwamba wao sio Mungu kiasi cha kuamua kukatisha maisha yangu na katika hili nitawachukulia hatua  wale wote walihusika katika uzushi huu kwa mujibu wa sheria"amesema  Tausi Milanzi.


Amesema kuwa swala la matumizi ya mitandao limekuwa kubwa sana kwa sasa hivyo lazima niwafikishe  katika vyombo vya sheria wote  waliohusika kusambaza ujumbe huu wa kifo changu jambo ambalo si kweli.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top