Uongozi wa Yanga, umewataka wachezaji wote wanaotaka kuondoka, kusema mapema.
Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesema klabu hiyo kongwe ingependa mambo kwenda kwa mpangilio.
“Kama kutakuwa na mchezaji ambaye mwalimu anaona hamhitaji, basi sisi tutafuata taratibu na kumueleza mapema kabisa.
“Kama kuna mchezaji anataka kuondoka, basi naye awe muungwana. Atueleze mapema na taratibu zifuatwe,” alisema.
Hata hivyo, Mkwasa alisema kwa sasa wameelekeza nguvu katika Ligi Kuu Bara na michuano ya Kombe la Shirikisho.
Katika msimamo wa Ligi Kuu Bara, Yanga iko katika nafasi ya pili nyuma ya Simba na ndiyo mabingwa watetezi lakini wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho.
Post a Comment
karibu kwa maoni