0



Huku Simba ikiwa imeingia kambini, beki Novaty Lufunga yeye hayupo kambini na wenzake na atakuwa akifanya tu mazoezi na wenzake.

Lufunga ameendelea kufanya mazoezi na wenzake akiwa nje ya kambi hiyo baada ya uamuzi wa benchi la ufundi kwa kuwa hautamtumia katika mechi ijayo.


Imeelezwa, Lufunga hatatumika kwa kuwa ana kadi tatu za njano. Hivyo wakati Simba ipo kambini yeye ataendelea na mazoezi tu na kuondoka.


Mratibu wa Simba, Abbas Ally ‘Gazza’ amelithibitisha hilo baada ya kuwepo taarifa kwamba Lufunga ametemwa kambini.


“Si kwamba ameachwa kwa sababu tofauti na zinazoelezwa. Lufunga ana kadi tatu za njano. Hivyo yeye anaendelea na mazoezi kama kawaida.



“Lakini baada ya mazoezi, anaondoka na kwenda nyumbani. Huwezi ukamchukua kambini mchezaji ambaye una uhakika hatatumika na hakuna kitu zaidi ya hicho,” alifafanua Gazza.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top