Kuna madai kutoka ndani ya familia ya Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kuwa, mama mzazi wa staa huyo, Sandra Kasim ‘Sanura’ hivi karibuni alifanya kikao kizito na mkaza mwanae, Zarinah Hassan ‘Zari’ kufuatia picha za mtalaka wake, Ivan Semwanga na mtoto wa pili wa Diamond, Nillan ambaye Zari ni mama yake mzazi, kutupiwa mitandanoni na watu kusema wamefanana.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, nia ya mama Diamond ilikuwa ni kutaka kujua nini kimefichika kati ya Zari na Ivan mpaka kunakuwa na ujasiri wa kutupiwa picha za Nillan akiwa sambamba na yeye na Diamond pia.
“Unajua mama siku zote ni mzazi mwenye uchungu sana. Sasa Ivan anachukua picha ya Nillan, anajiunganisha na yeye na Diamond anakuwa pembeni kisha anatupia kwenye mitandao, watu wanachangia, wanasema mtoto kafanana sana na jamaa huyo.
“Mama anajisikia vibaya, anahisi kama kuna kitu, huenda Zari anakijua hivyo ikabidi amuweke kikao na kumuuliza nini kimefichika baina yao?” kilisema chanzo hicho huku kikiomba hifadhi ya jina. Ikazidi kudaiwa kuwa, katika kikao hicho, mama Diamond alikumbusha kuwa, hii si mara ya kwanza kwa picha za Ivan kuwekwa mitandanoni kwani Zari alipojifungua Latifah ‘Tiffah’ mwaka juzi, pia picha zake na Ivan ziliwekwa mtandaoni na watu wakaanza kutupia maoni kuwa, wawili hao kama mapacha kabisa!
Hata hivyo, chanzo hicho hakikuweza kuweka wazi majibu ya Zari yalikuwa yapi, lakini kufuatia picha hizo, watu wamekuwa wakiweka maoni wakishauri Diamond kujiongeza kwa kusema kuwa, lisemwalo lipo kama halipo linakuja, inakuwaje picha za watoto wake ziwe gumzo kila Zari anapojifungua? Ili kupata ukweli wa madai ya kikao hicho, Amani juzi lilimtafuta mama Diamond kwa njia ya simu ili kumsikia anasemaje kuhusu hilo lakini baada ya kupokea simu na Amani kujitambulisha kwake, alikata simu.
Amani likampigia mara kadhaa likiamini kuwa, huenda simu ilikatika kwa bahati mbaya au alikuwa sehemu mbaya, lakini mama huyo hakupokea wala kujibu meseji aliyotumiwa ikiwa na maelezo yote.
Amani liliongea na Diamond na kumuuliza picha za Ivan, Nillan, Tiffah na yeye kutupwa mtandaoni na watu kusema wamefanana na jamaa huyo aishiye nchini Afrika Kusini ambapo alisema yeye ni baba na ndiye anayejua ukweli.
“Mimi ndiye baba, ndiye ninayejua ukweli wa watoto wale. Sipendi kujibu haya mambo kwa sababu nikijibu nitakuwa nampa kiki mtu mwingine bila sababu ya msingi. Kwa nini nimpe kiki mwingine? Ndiyo maana nakaa kimya tu lakini ukweli naujua mwenyewe,” alisema Diamond.
Kumekuwa na maneno ya chini kwa chini kutoka kwa watu mbalimbali wakitilia shaka ukaribu wa Ivan na Zari, wengine wakisema bado upo kwa sababu ya watoto, wengine wakisema upo kwa maana ya mapenzi. Ivan na Zari wameshazaa watoto watatu ambao ni Pinto, Didy na Quincy.
Jumla kwa sasa, Zari ana watoto watano, wa kike mmoja. Madai mengine ambayo yanachipuka kwa kasi ni ndoa ya Ivan na Zari kama iliwahi kuvunjika kisheria ambapo baadhi ya watu wanasema huenda Diamond akawa anaingizwa chaka kwani kama hakuna talaka, kisheria Tiffah na Nillan pia ni watoto wa Ivan, lakini Diamond aliwahi kusema kuwa, Zari yupo singo na hana pingamizi ya kuwa na yeye na ndoa yao itafungwa hivi karibuni.
Post a Comment
karibu kwa maoni