0
WAFUGAJI wa mkoa wa MANYARA wamesema wanashindwa kuuza baadhi ya mifugo yao ili kununua chakula kipindi  hiki cha ukame kutokana na mifugo hiyo kuathirika  kwa kukosa majani na kusababisha kushuka bei katika soko.

Kutokana na hali hiyo baadhi ya baadhi ya wananchi wanalazimika kutumia maziwa kama chakula chao cha kila siku huku wale wasio na ng’ombe wakikabiliwa na hali mbaya zaidi.

Kijiji cha ESHKESHI katika tarafa ya HAYDOM wilayani MBULU ni miongoni mwa maeneo ya Jamii ya Wafugaji yaliyoathirika kwa ukame kutokana na mvua kuchelewa kuanza kunyesha.

Baadhi ya wadau ikiwemo kampuni ya  BARGWEKA FARMERS imetoa Gunia 250 za mahindi zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 37 kwa kaya zilizoathirika.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top