0
Image result for BANGI
Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya KITETO mkoani MANYARA imeng’oa mimea ya bangi katika moja ya mashamba ya wananchi wa kijiji cha KIMANA wilayani humo.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mkuu wa wilaya ya KITETO Mhandisi TUMAIN MAGESSA  amesema mmiliki wa shamba la bangi katika kijiji cha KIMANA, kata ya PARTIMBO, GEORGE MUSSA  amekiri kuzalisha bangi kwa muda mrefu kwa madai kuwa inamwingia kipato.

Mkuu wa wilaya hiyo ya KITETO amesema oparesheni hiyo ni endelevu ili kukomesha kilimo na matumizi ya bangi katika wilaya hiyo.

Aidha wakati wa oparesheni ya kung’oa bangi pia imekamatwa bunduki moja iliyokuwa inamilikiwa kinyume cha sheria.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top